Patrick Mutesa Mafisango, aliyevalia Jezi Namba 30 akiwa amegeuka (nyuma ya Kocha wa timu hiyo, akiwa na kikosi cha Simba siku ya mechi na watani wao wa Jadi. ************************************** |
JEZI namba 30, iliyokuwa ikivaliwa na aliyekuwa Kiungo mkabaji wa timu ya Simba Sports Club, Patrick Mutesa Mafisango, aliyefariki alfajiri ya jana maeneo ya Keko kwa ajali ya gari, imeelezwa kuwa haitatumika tena katika kikosi cha timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kumuenzi kwa heshima
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Ismail Aden Rage, wakati akisoma taarifa maalum ya salam kutoka Klabu hiyo, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Mafisango zilizofanyika katika viwanja vya TCC, Chang'ombe leo, ambapo hata hivyo Rage alishindwa kumalizia taarifa hiyo kutokana na uchungu na taarifa hiyo ikamaliziwa kusomwa na Kaburu.
Katika shughuli hiyo, wameanguka watu kadhaa kutokana na kushindwa kuvumilia ambapo miongoni mwao alikuwa ni Kiungo wa timu ya Simba mwenye vituko Lukuki kama Baloteli, Haruna Moshi 'Boban', ambaye alitinga anga hizo akiwa amevaa Kandambili za rangi ya Bluu chini, huku akiwa ametinga Tisheti ya Kilimanjaro, aambayo ni sare ya wachezaji wa timu ya Taifa waliofika eneo hilo, ambaye aliwasili mahala hapo akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya Taifa.
Boban, aliinuliwa na wachezaji wenzake wa Simba wakati wakielekea kuaga na kuungana nao kabla ya kikosi chake cha timu ya Taifa na alipofika mbele ya Jneza alishindwa kuvumilia na kulegea na kupoteza nguvu na kusaidiwa na wenzake.
WENGI WAMUAGA MAFISANGO KWA HUZUNI LEO.
Wachezaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Juma Nyoso, John Boko (mbele) na wenzao wakiwa wamebeba Jeneza la mwili wa marehemu, Patric Mafisango wakati wa shughuli za kuaga mwili na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika katika Viwanja vya TCC, Chang'ombe Dar es Salaam , leo mchana.
Juma Kaseja, akisaidiwa na Mtangazaji wa Clouds Fm, Ibahim Maestro, ambaye pia ni Mjumbe wa Klabu hiyo, wakati wakitoa heshima zao za mwisho.
Mdogo wa marehemu akilia na kusaidiwa wakati wa kuaaga mwili wa marehemu katika viwanja vya Sigara Dar es Salaam.
Nurdin Bakari na Mrisho Ngasa, wakipita kutoa heshima zao za mwisho.
Mwenyekiti wa Simba, Aden Ismail Rage na Haruna Moshi 'Boban', wakipita kutoa heshima za mwisho.
Huyu ni miongoni mwa waombolezaji waliokuwapo eneo hilo ambaye alianguka kwa kupoteza nguvu, akiwa amebebwa kupelekwa kupatiwa huduma ya kwanza.
No comments:
Post a Comment