Habari za Punde

*SPIKA WA BUNGE MHE. ANNE MAKINDA NA MWENYEJI WAKE SPIKA WA JAPAN TAKAHIRO YOKOMICHI WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIBUNGE

 Spika wa Bunge la Japan Takahiro Yokomichi ( kulia) akimkalibisha Spika wa Bunge katika Bunge la Japan kwa lengo la kufanya mazungumzo kuimarisha ushrikiano baina ya mabunge hayo mawili.

 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (katikati) akimsikiliza kwa Makini mwenyeji wake Spika wa Bunge la Japan Mhe. Takahiro Yokomichi wakati wa kikao cha pamoja kati ya ujumbe wa  Bunge la Tanzania na Japan walipo kutana Bungeni japan leo. Kulia kwa Spika ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, ardhi na Mazingira Mhe. James Lembeli na Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Anne Kilango. Ujumbe wa Bunge la Tanzania upo Japan kwa mwaliko maalum na Bunge la Japan kwa lengo la kujadili na kuimarisha ushirikiano baina ya Mabunge hayo mawili.
 Ujumbe wa Bunge la Tanzania ukiongozwa na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya Bunge la Japan na ujumbe wa Bunge la Japan ambao uliongozwa na Mwenyeji wake Spika wa Japan Mhe. Takahiro Yokomichi mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja kilichojadili namna ya kuimarisha ushirikiano na mahusiano kati ya Mabunge ya Nchi hizi Mbili.
 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akimkabidhi zawadi ya picha yenye wanyama (the Big Five animals) Spika wa Bunge la Ushauri la Japan (President of House of Councilors) Mhe. Kenji Hirata wakati alipomtembelea Ofisi kwake baada ya kumalizika kwa kikao kati ya Ujumbe wa Bunge la Japan  na Tanzania.

Spika wa Bunge akifanya mahojiano na Mwakilishi wa TBC aliyeko Radio Japan – idhaa ya Kiswahili (NHK) Anna Kwambaza  mara baada ya Spika na Ujumbe wake kumaliza kikao na Mwenyeji wake Spika wa Japan, leo. Picha na Owen Mwandumbya

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.