Habari za Punde

*KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF YATOA MAAMUZI NA KUIAGIZA YANGA

Kamati ya uchaguzi ya TFF kupitia kikao chake kilichofanyika leo mchana, ilijadili mustakabali wa nafasi za uongozi ndani ya Klabu ya Yanga na kupokea ushauri wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi ya za wachezaji ya TFF, kufuatia kujiuzulu kwa wajumbe wanane (8) na kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Kamati ya Uongozi ya TFF imetoa ufafanuzi na kuiagiza Kamati ya Uchaguzi ya Yanga mambo yafuatayo:-

(1):- Kamati ya Uchaguzi ya Yanga ianze mara moja mchakato wa kujaza nafasi zilizowazi za Wajumbe wa kuchaguliwa wa  Kamati ya Utendaji waliojiuzulu kwa mujibu wa Katiba ya Yanga Ibara ya 28, na nafasi iliyowazi kutokana na kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.

(2):- Mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi uanze Juni 1, mwaka huu, na ufanyike kwa kuzingatia kikamilifu Kanuni za uchaguzi za Wanachama TFF.

(3):- Uchaguzi wa Viongozi wa Yanga kujaza nafasi zilizowazi ufanyike Julai 15, mwaka huu katika mkutano wa uchazi, mahali patakapopangwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Yanga.

(4):- Mkutano Mkuu wa uchaguzi utakuwa na Ajenda moja tu ya uchaguzi 'kujaza nafasi zilizowazi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa kuchaguliwa.

(5):- Kamati ya uchaguzi ya Yanga, iandae na isimamie shughuli za uchaguzi kwa kuishirikisha Sekretarieti ya Yanga kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za  Wanachama wa TFF, chini ya usimamizi na maelekezo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kwa mujibu wa Katiba ya TFF Ibara ya 49 (1) na Katiba ya Yanga Ibara ya 45 (1) na (2).

IMETOLEWA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
DEOGRATIAS LYATTO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.