Habari za Punde

* TWIGA STARS KUPAA MEI 24 KWENDA ETHIOPIA KUKIPIGA MEI 27


Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka nchini Mei 24 mwaka huu kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwenda Addis Ababa kwa ajili ya  
mechi ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia.

Mechi hiyo itachezwa Mei 27 mwaka huu.

 Msafara wa Twiga Stars utakuwa na watu 25 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Lina Kessy ndiye atakayeongoza msafara huo.

Twiga Stars itarejea nyumbani Mei 28 mwaka huu kusubiri mechi ya marudiano itakayochezwa Juni 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mshindi ndiye atakayepata tiketi ya kucheza Fainali za Nane za AWC zitakazochezwa Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.

  TWIGA STARS, BANYANA ZAINGIZA MIL 8/-
Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Twiga Stars na Afrika Kusini (Banyana Banyana) iliyofanyika Mei 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 8,012,000.

Mapato hayo yametokana na washabiki 6,418 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 1,000, sh. 5,000 na sh. 1,000. Washabiki 6,057 walikata tiketi z ash. 1,000.

Asilimia 18 ya mapato ambayo ni sh. 1,222,169 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 1,560,000), waamuzi (sh. 650,000), usafi na ulinzi (sh. 1,000,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 500,000) na umeme (sh. 300,000).

 Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 475,966, asilimia 10 ya uwanja sh. 237,983, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 118,992 na asilimia 65 ya TFF (sh. 1,546,890).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.