Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Dkt. Fenella Mukangara, amepata ajali ya Gari maeneo ya Nzega mkoani Tabora, wakati akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza katika shughuli za kikazi ambako alialikwa kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya Taifa ya mchezo wa vishale maarufu kama (DARTS). Imeelezwa kuwa katika ajali hiyo Dkt. Mukangara, amepata majeraha madogo madogo tu na watu wote walioambatana naye wamesalimika.
DC MSANDO AAGIZA KUFUFULIWA VISIMA VINNE MBURAHATI, HUDUMA YA MAJI KUREJEA
-
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC), Mheshimiwa Abert Msando ametembelea na
kukagua hali ya huduma ya upatikanaji maji kata ya Mburahati wilayani humo
huku akito...
1 hour ago

No comments:
Post a Comment