Habari za Punde

*MASHINDANO YA VISHALE YA AFRIKA MASHARIKI YAFUNGULIWA JIJINI MWANZA

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, akicheza mchezo wa Vishale (Darts) kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya wazi ya mchezo huo (Tanzania Intarnational Open Darts Championships) kwa niaba ya Waziri wa Habari, ajira Utamaduni na michezo, Dkt. Mukangara, aliyepata ajali mkoani Tabora jana wakati akiwa safarini kutua jijini Mwanza kwa ajili ya kufungua mashindano hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama.
***************************************
MASHINDANO  ya Vishale (Darts) ya Wazi yamefunguliwa rasmi jijini Mwanza  leo na Meneja wa  Bia ya Safarai Lager, Oscar Shelukindo, kwa niaba ya Waziri wa Habari Dkt. Fenella Mukangara, aliyepata ajali mkoani Tabora jana wakati akiwa safarini kutua jijini Mwanza kwa ajili ya kufungua mashindano hayo.

Akizungumza na wachezaji washiriki wa mchezo huo, Mejeja Oscar Shelukindo, alisema kuwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imekuwa ikidhamini mashindano ya vishale kwa muda mrefu sasa kwa kutambua umuhimu wa mchezo huo kwa wapenzi na mashabikmi  kwa ujumla na itaendelea kudhamini mchezo huu katika mashindano mbalimbali ya ndani na yale ya kimataifa ili kuinua mchezo huo.

Shelukindo, alisema Darts ni moja ya michezo ambao inatakiwa ipewe kipaumbele kama michezo mingine kama Safari Lager inavyofanya kujitolea kuudhamini mchezo huo unaofanyika katika Hoteli ya Monarch jijini Mwanza kwa siku nne, ambapo mashindano hayo ya Afrika Mashariki  yanazishirikisha jumla ya nchi nne za Tanzania, Kienya , Uganda na Rwanda.


 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.