Marcio Maximo, ambaye kwa sasa ni Kocha wa timu ya Democrata F.C ya mjini Rio de Jeneiro Brazil, anatarajia kuwasili nchini siku ya jumapili kwa Ndege ya Emirates, akiongozana na Kocha msaidizi wake kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuifundisha Timu ya Yanga.
Awali iliripotiwa kuwa Kocha huyo angewasili hii leo, lakini kutokana na maombi ya Klabu yake anayoifundisha kwa sasa ya Democrata F.C, kumtaka kutoondoka kwa haraka ndiyo yamemfanya kusogeza siku ya kuwasili nchini.
Akiungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, kwa njia ya simu, Msemaji wa Timu ya Yanga, Louis Sendeu, amesema kuwa baada ya kocha huyo kubwa na uongozi wa Klabu hiyo kuwaandalia na kuwaachia Program za kuendelea nazo kabla ya kupata Kocha mpya atakayeshika nafasi yako katika kikosi hicho.
Aidha imeelezwa kuwa Baada ya Kocha huyo kuwasili nchini kabla ya kusaini mkataba wake kwanza atakutanishwa na Yusuph Manji kwa mazungumzo na kisha baada ya mazungumzo na makubaliano ndipo atasaini mkataba huo.
''Kila kitu kuhusu ujioa wa Maximo kimekamilika na bado Maximo ameendelea kusisitiza kuwa anamhitaji Mrisho Ngasa, katika kikosi chake jambo ambalo bado Uongozi wa Yanga unalifanyia kazi'', alisema Sendeu
No comments:
Post a Comment