Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Kyela mkoani Mbeya, MAISHA SAMSON, ameahidi kumtwanga mpinzani wake THOMAS
MASHALI, kwa knock-out ya raundi ya 9 katika pambano lao litakalo fanyika Juni 6 mwaka huu, katika ukumbi wa FRIENDs- CORNER Jijini Dar-es-salaam.
Pambano hilo la raundi 10 Thomas Mashali, atakuwa anatetea ubingwa wake wa taifa unaotambuliwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini Tanzania chini ya rais wake YASSIN ABDALLAH -USTAADH.
Mabondia hao watapigana uzito wa kati (middle kilo 72.5), ambapo Maisha, amesema anasikia sana sifa za mashali anayejiita SIMBA ASIYEFUGIKA, lakini ajuwe siku ya pambano atamuonyesha kazi ngumu na akamtaka mashali awe mvumilivu ulingoni kwani yeye ni tofauti na mabondia alioishakutana nano.
Maisha amepigana jumla ya mapambano 8 ambayo yote alishinda na kutamba kuwa amekutana na mabondia wajeuli zaidi ya THOMAS MASSHALI ,kutoka nchi za Malawi ,Zambia na Namibia, ''hivyo siona sababu kwa nini nishindwe kumpiga THOMAS MASHALI na kumpora mkanda wake na kurudi nao Kyela''. alijigamba bondia huyo kutoka mkoani Mbeya.
Maisha aliwataka wakazi wa Mbeya waishio jijini Dar es Salaam, kujitokeza kwa wingi kumshangilia siku hiyo.
Wakati huo huo, mabondia wa ngumi za kulipwa tarehe 30-06-2012 watakutana ukumbi wa Community Center, kupambana na mabondia kutoka Dar-es-salaam katika pambano lenye lengo la kumuenzi bondia magoma shabaani aliyefariki dunia hivi karibuni.
Promota wa pambano hilo, Ally Mwazoa, amesema sehemu ya mapato ya mapambano hayo, yataisaidia familia ya magoma shabani.
''Ratiba hii itakuwa ya kuendelea na siyo ya muda ,tutajitahidi kufanya hivyo kila baada ya miezi 6 kwani magoma ameacha familia ambayo ilikuwa inamtegemea hivyo ni wajibu wetu sisi familia ya ngumi za kulipwa tuendelee kuwa pamoja na familia yake''. alisema Ally
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
No comments:
Post a Comment