Habari za Punde

*PAMOJA NA AGIZO LA SERIKALI, BADO HUDUMA YA JIWE INATOKA MAHALA HAPA

 Mama Mjasiliamali, akiponda kokoto kwa katika eneo la Bonde la Tegeta, mahala ambapo Serikali ilipiga marufuku zoezi la kuendele kuchimba Mawe na Kokoto,  Mama huyu huponda Kokoto na kulipwa ujira na bosi wake kulingana na kiasi alichoponda kwa siku, jambo ambalo linawafanya wenye maeneo haya kuendelea na zoezi hilo kama kawaida. Na sasa watu walio na maeneo mahala hapa wamekuwa wakiuza maeneo ya Viwanja kwa wananchi, ambao baadhi yao wameshuhudiwa na mtandao huu wakiendelea na ujenzi wa nyumba mahala hapa. Je wahusika mpo?? au mnasubiri wakianza kuishi ndiyo muanze kuwatimua??
 Hizi ni baadhi ya nyumba zilizojengwa na zinazoendelea kujengwa na wageni waliouziwa maeneo katika eneo hili.
 Baadhi ya wenye maeneo ya Mawe, wakiendelea kuchimba mawe, mahala hapa.
Hawa jamaa nao, wanashusha udongo huu hadi wafikie levo ya Jiwe jeupe linaloonekana ili waanze kuchimba mawe. Imeelezwa kuwa kazi hii ya kuondoa dongo jekundu hadi kufikia jiwe kama wanavyoonekana jamaa hawa inachukua siku mbili hadi tatu kwa watu hawa wawili tu wanaoonekana juu ya kichuguu hicho.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.