Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour) iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania Marekani. Hii ni mara ya pili kufanyika ziara kama hii, ambapo pamoja na kuwakaribisha tena Rais Kikwete alisema amefurahishwa sana kwa wageni hao kuchagua kutembelea hifadhi za wanyama za kusini mwa nchi (Selous na Ruaha) zenye wanyama wengi na vivutio ambavyo havipatikani kwingine kokote kama vile makundi ya mbwa mwitu ambayo kwa muda mrefu sasa yametoweka mbuga za Kaskazini.Picha na IKULU
Tanzania mgeni rasmi Maonesho ya Ufugaji Nyuki Afrika nchini Algeria
-
Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe Mobhare Matinyi, akizungumza na
vyombo vya habari vya Algeria wakati akitangaza kuwa Serikali ya Jamhuri ya
Muun...
4 hours ago

No comments:
Post a Comment