Habari za Punde

*SAFARI LAGER YATANGAZA KUDHAMINI MASHINDANO YA DARTS MKOA WA DAR ES SALAAM 2012 (DADA CUP 2012).


Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akiashilia ufunguzi rasmi wa mashindano ya Darts Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu udhamini wa mashindano hayo kwenye Ukumbi wa Moshi Hotel Manzese Dar es Salaam jana.Picha na Bhujaga Maziku.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa,Gesase Waigama.

***********************************

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi kudhamini mashindano ya Darts Mkoa wa Dar es Salaam yanayotambulika kama “DAR ES SALAAM DARTS ASSOCIATION TOURNAMENT 2012” yanayotarajiwa kuanza rasmi kesho Juni 15 na kumalizika jumapili Juni 16,2012, ukumbi wa Moshi Hotel jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo amesema Safari Lager imesaidia kiasi cha fedha kuendesha mashindano hayo ikiwa ni pamoja na zawadi za vikombe na pesa taslimu.“Safari Lager inaendeleza lengo lake la kusaidia kukuza zaidi mchezo wa Darts hapa Tanzania’, alisema Bw. Shelukindo. Safari Lager imekuwa ikidhamini mashindano mbalimbali ya mchezo wa Darts ikiwa ni pamoja na kudhamini timu ya taifa hapa ndani na nje ya nchi. Safari Lager imegawa pia vifaa vya michezo kwa maeneo mbalimbali ya kuchezea Darts Dar Es Salaam na mikoani.
Naye mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Darts cha Taifa (TADA) Bw. Gesase N. Waigama, ambaye pia ni raisi wa shirikisho la Darts Afrika Mashariki alisema timu shiriki katika mashindano haya ni Temeke,Ilala na Kinondoni ambazo zimeunda kombania ya Wilala kila moja.Waigama akiendelea kusema kwamba, “Tunawashukuru sana TBL kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kutupa udhamini mara kwa mara, kwa niaba ya wacheza Darts tunaahidi kujitahidi kuhakikisha kiwango kinakua na tunafanya vizuri siku hadi siku kwani hilo ndio lengo hasa la Safari Lager”.
Na kumalizia bwana Shelukindo alisema, “Tunaendelea kuwashukuru wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, ni kwa mchango wao ndio na sisi tunaweza kusaidia michezo mbalimbali hapa Tanzania. Ikumbukwe pia kwamba Safari Lager inasaidia sana katika kukua kwa mchezo wa Pool kwa sasa, tuna mashindano ya Pool yatakayoanza wiki ijayo na kuendelea hado Mwezi September, yote haya ni kutokana na mchango mzuri kutoka kwa wateja wetu na tunashukuru sana kwa hilo”

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.