Gari aina ya Fuso likiwa limebeba Kontena kubwa na refu zaidi ya uwezo wake huku likipita katika barabara ya Fuoni mjini Zanzibar huku likisababisha msululu mkubwa wa foleni za magari yaliyokuwa yakitokea nyuma yake kutokana na gari hilo kwenda mwendo mdogo zaidi ili kuepuka kuangusha mzigo huu.
Kontena hili kama linavyoonekana likiwa limezidi Bodi ya gari lililolibeba na kuhatarisha magari mengine yanayotoka nyuma yake na mengine yakiogopa kulipita kutokana na kuyumba kwa kutofungwa kikamilifu.
Hata hivyo Roli hili kote lilikopita lilikuwa likipishana na askari wa usalama Barabarani ambao walikuwa wakilitazama na likipia huku wao wakiendelea na shughuli zao, jambo ambalo limezua maswali mengi kwa baadhi ya madereva waliokuwa nyuma ya Foso hilo.
Sasa endapo Roli hili likisababisha maafa kwa ajali ama vinginevyo kutokana na usafirishaji wa aina hii ni nani wa kulaumiwa, dereva, Askari wa usalama Barabarani, Sheria za usalama Barabarani ama mwenye mali?
Kulia ni Askari wa usalama Barabarani wakiendelea na mishe mishe zao huku Roli hili likikatiza na kuendelea na safari zake.
Hebu ona lilivyozidi nyuma ni HATARI tupu.
No comments:
Post a Comment