Habari za Punde

*MIKOA MITANO YAKAMILISHA MASHINDANO YA SAFARI POOL TAIFA NGAZI YA MKOA

Bingwa wa mchezo wa pool mmoja mmoja (singles) Mkoa wa Shinyanga, Ndala Ndefu, akicheza dhidi ya mpinzani wake Majaliwa Cyipilian, wakati wa mashindano Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika Klabu ya Garden mwishoni mwa wiki.
****************************
MIKOA mitano kati ya 16 inayoshiriki mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mikoa, imekamilisha fainali zake mwishoni mwa wiki hii kwa kupata klabu,mchezaji mmoja mmoja (single) Kwa upande wa Wanaume na wanawake.
Katika mashindano hayo, mshindi wa kwanza alijinyakulia Shilingi 700,000/=, mshindi wa kwanza wa kiume alipata shilingi 350,000/= na wa kike 250,000/= pamoja na zawadi nyingine kwa washindi wa pili na tatu.
Walioibuka mabingwa katika mashindano hayo ni Mkoa wa Shinyanga kutoka Klabu ya New Stand, mchezaji wa single wanaume ni Ndala Ndefu na singles wanawake ni Sada Tuwa, Mkoa wa Kagera mshindi wa timu ni klabu ya Balele,singles wanaume ni  Hakimu Mzamili na singels wanawake ni Angel Mfaume
Tabora mabingwa ni Klabu ya Texas, singles wanaume ni Waziri Ally na singles wanawake ni Angel Mfaume wakati Manyara mabingwa ni Klabu ya Janja Wild, singles wanaume ni Ally Nada na singles wanawake ni Chiku Mohamed.
Kilimanjaro mabingwa ni klabu ya Mbosho,singles wanaume ni Teter George na singles wanawake ni Cecilia Kileo.
Washindi hawa watawakilisha mikoa yao katika mashindano ya Taifa ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Semptemba jijini Mwanza kwa kushilikisha Mikoa 16 ya Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.