Habari za Punde

*TWANGA PEPETA KUWACHEZESHA KISIGINO MISS SINZA, KAMATI YA MISS TANZANIA KUWATEMBELEA KAMBINI KESHO

Kamati ya Miss Tanzania kutembelea kambi Kesho

Na Mwandishi Wetu
BENDI ya African Stars (Twanga Pepeta) itapamba shindano la kumsaka mrembo wa Redds Miss Sinza 2012 lillopangwa kufanyika Ijumaa ya wiki hii kwenye ukumbi wa Mawela Social (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hoteli ya Vatican City Sinza.

Katika maandalizi na kusherehesha shindano hilo, kesho Kamati ya Miss Tanzania itawatembelea warembo hao  kwa lengo la ‘kuwafunda’ kabla ya kupanda jukwaani siku ya Ijumaa.

Mratibu wa kampuni  ya Calapy Entertainment, Majuto Omary, alisema kuwa Twanga Pepeta imeandaa zawadi kwa mashabiki wake na wale wa fani ya urembo kwa kuwapa uhondo wa nyimbo mbili mpya ambazo zitakuwa zinasikika kwa mara ya kwanza katika Jukwaa la Miss Sinza.

Nyimbo hizo ni Mapambano ya Maslahi, uliotungwa na Muumin Mwinjuma, Shamba la Twanga ambao umetungwa na Greyson Semsekwa na mmoja ambao haujapewa jina uliotungwa na Jumanne Saidi ambaye ni rapa wa bendi hiyo aliyefunga ndoa na mnenguaji wa bendi hiyo, Asha Sharapova, siku za hivi karibuni.

Alisema kuwa nyimbo hizo ni zawadi kwa mashabiki wa Twanga wa Sinza na vitongoji  vyake  kwani bendi hiyo haijafanya shoo katika maeneo hayo kwa kipindi kirefu.

“Tunatarajia kuwa na shoo nzuri kutoka kwa warembo na bendi ya Twanga Pepeta ambayo mwaka huu imeshinda tuzo mbili katika tuzo za muziki Tanzania,” alisema.

Kuhusiana na ziara ya Kampuni ya Lino International Agency, Majuto alisema kuwa Lundenga na wenzake watafanya mazungumzo na warembo hao baada ya mazoezi yao ya pamoja.

Alisema kuwa ziara hiyo ni moja ya faraja kwa warembo na kamati ya Miss Sinza kutokana na ukweli kuwa ujio wao ni wa Baraka na hitimisho la mashindano ya vitongoji nchini.

“Miss Sinza ndiyo inafunga pazia la mashindano ya Vitongoji (vituo) nchini, Lundenga na wenzake wanakuja kutoa baraka zao kabla ya kuanza pilikapilika za Redds Miss Tanzania,” alisema.

Shindano hilo lililodhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Kidoti Fashion, Clouds Entertainment, sufianimafoto.blogspot.com, Lady Pepeta na flexi P, Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake  Point na Jackz Cosmetics Kinondoni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.