Habari za Punde

*MTOTO AISHIE KATIKA MAZINGIRA MAGUMU AONGOZA MTIHANI WA DARASA LA SABA

 Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Msingi Ungindoni wilayani  Temeke anayelelewa katika Kituo cha New hope Family, Joel Joseph,  akipokea zawadi ya vitabu na madaftari, kutoka kwa mshauri wa Kituo hicho, Michael Lugendo, baada ya kufanya  vizuri katika mtihani wake wa kumaliza muhula wa darasa la saba  na kushika nafasi ya kwanza katika shule ya Msingi Ungindoni wilayani  Temeke . Kushoto ni Mlezi Kituo hicho Mariam Pius, Mwenyekiti wa Kituo Omar Rajab (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa Kituo hicho Hashim Yusuf Mahmoud (kulia).
Mwenyekiti wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha New Hope Family, Omar Rajab (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es alaam, kuhusu mtoto Joel Joseph (hayupo pichani)  kutoka Kituo hicho alivyofanya vizuri katika masomo yake na mtihani wa kumaliza muhula na kushika nafasi ya kwanza darasa la saba katika shule ya Msingi Ungindoni wilayani  Temeke . Wengine ni Mlezi Kituo hicho Mariam Pius(kushoto) na Katibu Mkuu wa Kituo hicho Hashim Yusuf Mahmoud (kulia). Picha na MAELEZO_ Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.