Beki wa timu ya APR ya Rwanda, Mbuyu Twite (ushoto) akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi, ambaye ni mfungaji pekee wa mabao 2 katika mchezo wa timu hizo mbili uliomalizika hivi punde katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuifanya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya APR.
Mabingwa hao watetezi wa Kombe la Kagame Yanga sasa wameshika nafasi ya pili katika michuano hiyo nyuma ya Atletico na wa tatu wakiwa ni APR. Yanga inategemea kucheza na mshind wa pili wa kundi B, ambaye anaweza kuwa ni kati ya Azam, Mafunzo ama Tusker, kutokana na kuwa katika kundi hilo hakuna timu iliyokwisha kwalifai mpaka sasa.
Bahanuz, akishangilia bao lake la kwanza.
Bahanuz, akipongezwa na wachezaji wenzake Hamis Kiiza (aliyembeba) na Haruna Niyonzima, baada ya kufunga bao la pili.
Nizar Khalfan (katikati) akidhibitiwa na mabeki wa APR wakati wa mchezo huo.
Said Bahanuzi, akiruka kwanja la beki wa APR wakati wa mchezo huo, ambpo Bahanuzi ameonekana kung'ara huku akikabwa na mabeki wengi kutokana na uchezaji wake wa 'sitaki nataka', ambapo wengi wamefananisha uchezaji wake na Mshambuliaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta.
No comments:
Post a Comment