Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya wabunge nje ya ukumbi wa Bunge leo, mjini Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza (kushoto aliyenyoosha mkono) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndasa katika ofisi za Bunge mjini Dodoma leo, baada ya kuwasilisha kauli ya Serikali kuhusu utaratibu wa Ruzuku ya Pembejeo kwa Wakulima kwa mwaka 2012/2013. Katikati ni Naibu wake Adam Malima.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza(kulia aliyegeuka) akisikiliza jambo kutoka kwa Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo na katikati ni Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndasa katika ofisi za Bunge mjini Dodoma leo, baada ya kuwasilisha kauli ya Serikali kuhusu utaratibu wa Ruzuku ya Pembejeo kwa Wakulima kwa mwaka 2012/2013. Picha Zote na Magreth Kinabo- MAELEZO
No comments:
Post a Comment