Habari za Punde

*MBIO ZA MBUZI ZA HISANI DAR ES SALAAM 2012


 Watoto wakishindana kuvuta kamba wakati wa mashindano ya mbio za mbuzi
ya hisani ya mwaka jana.
****************************************
 Mbio za Mbuzi za Hisani Dar es Salaam 2012 (2012 Dar es Salaam Charity Goat Races)

‘Mbuzi Mmoja tu Anaweza Kuleta Mabadiliko’                   
Matayarisho ya mwisho ya Mashindano ya 12 ya Mbio za Hisani za Mbuzi yatakayofanyika Septemba 1 mwaka huu jijini Dar es Salaam yanaendelea.

Tukio hilo la kifamilia linalofanyika kila mwaka tayari limeshafanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi milioni 544 (zaidi ya dola 345,000) kutoka kwa karibu makundi 50 ya wahisani wa ndani tangu lilipoanza mwaka 2001. (Tazama maelezo chini kwa mbio za mwaka huu.)

Zaidi ya watu 3,000 hushiriki kila mwaka, huku pia wakijifurahisha kwa kutabiri mbuzi atakayeshinda, wakishiriki kwenye mashindano ya mavazi yenye muonekano wa aina yake na kujiaribu ladha ya vyakula mbalimbali vya kiasili na vinywaji wakiwa na familia na marafiki zao.

Yeyote anaweza kushiriki na kushinda zawadi mbalimbali za kuvutia, ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa kwa mwaka huu kutoka Shirika la Ndege la Uingereza (British Airways) tiketi ya kwenda na kurudi Uingereza. (Tazama orodha nzima ya zawadi chini.)

Watoto, kuanzia wanaotambaa na kuendelea, nao watapata fursa nzuri ya kufurahi kwenye eneo maalumu lililodhaminiwa na Game kwa kila wakitakacho. Kutakuwapo michezo ya kufurahisha, kupakwa rangi usoni, michezo ya sanaa, mashindano ya mavazi ya watoto na burudani kutoka Kituo cha Kigamboni Community Centre (tazama maelezo).

Mwanzilishi wa mbio za Dar Charity Goats Race, Paul Joynson-Hicks anasema: “Nadhani inafurahisha kuona kuwa wazo la kuchekesha kama hili la mbio za mbuzi Iimegeuka na kuwa tukio kubwa hapa Dar.

“Si tu kwamba tunakusanya mamilioni ya fedha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za hisani na kusaidia makundi mbalimbali, kubadilisha kabisa maisha ya watu, lakini pia tunalifanya tukio hili kwa namna ambayo inavuta hisia za wengi huku likiwafurahisha.”

Mashindano ya mwaka huu yatafanyika kuanzia saa sita mchana hadi saa 11.30 jioni, kwenye viwanja vya The Green, Barabara ya Kenyatta.

‘Dar Charity Goat Races’ inaandaliwa na kamati ya watu waliojitolea, pamoja na mkazi wa siku nyingi wa jiji hili, Bi. Karen Stanley ambaye ndiye kinara wa tukio hili.

Mama huyo alisema: “Ninafuraha sana kushuhudia jambo hili likiendelea kukua mwaka hadi mwaka likiwa na muonekano wa kuvutia kwa sasa.

“Ukarimu wa wadhamini, wakubwa kwa wadogo, unamaanisha kuwa tunaweza kukusanya kiasi kikubwa cha fedha ambacho baadaye hutolewa kwa watu ambao kweli wanahitaji kusaidiwa.

“Haya yasingeweza kufanyika bila wao, hasa wale wanaolipa ili wamiliki mashindano haya. Wamiliki wa mbio za mwaka huu ni Southern Sun, British Airways, Coca-Cola, Tanzanian Breweries Limited, British Gas, aetna na Mantra Tanzania.”

Tiketi moja ni Shilingi 5,000 na zitauzwa getini. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti www.goatraces.com, au tuma barua pepe: goatraces@goatraces.com au piga simu 0755 555 900.

Kwa waandishi wa habari wasiliana na Peter Mgongo kwa simu 0784 765454 au barua pepe mgongo@gmail.com. Lakini kwa ujumla unaweza kuwasiliana na Emma Pearson (mjumbe wa kamati anayeshugulikia vyombo vya habari na mawasiliano ya umma) kwa simu 0768 912933 au barua pepe ekpea@yahoo.co.uk

Maelezo kwa Wahariri:

  1. Mwenyekiti wa Kamati ya ‘Goat Races’, Karen Stanley anapatikana kwa mahojiano ikiwa itahitajika.
  1. Picha pia zinapatikana kwa maombi rasmi.
  1. Jinsi mbio hizo zinavyofanyika:
*Kuna aina saba za mashindano. Kila moja hudhaminiwa na wamiliki wa mbio hizo ambao kwa mwaka huu ni Southern Sun, British Airways, Coca-Cola, Tanzania Breweries Limited, British Gas, aetna na Mantra Tanzania.

*Hawa humlipia mbuzi mmoja katika shindano moja. Mbuzi wao akishinda, wanakuwa na nafasi ya kupata zawadi kubwa. Wengi huungana na rafiki au jamaa zao na kuwa wamiliki wa pamoja wa mbuzi.

*Wote hupata nafasi ya kuingia kwenye eneo maalumu na kupata nafasi nzuri ya kumshangilia mbuzi wao, na kupata vinywaji na chakula bure kwa hisani ya Southern Sun Hotel, Tanzania Breweries Ltd, Tanzania Distilleries Ltd, RednWhite na Coca-Cola.

  1. Wahisani wa mwaka huu ni:
·         Africa's Children - Africa's Future
·         BibiJann's Centre
·         Diocese of Central Tanganyika
·         Foxes' NGO
·         Kidzcare Tanzania
·         Kigamboni Community Centre
·         Molly's Network
·         United Planet
·         Zanzibar Outreach Program 

  1. Kituo cha Kigamboni Community Centre – Hushughulikia umasikini na masuala ya afya kwa kutoa elimu ya bure kwa watoto walio kwenye mazingira magumu. Wana mambo mengine kadhaa wanayoyafanya ikiwa ni pamoja na masuala ya utamaduni kama maigizo, ngoma za asili na za kisasa, soka, muziki na sarakasi.
  1. Zawadi za mwaka huu ni:
·         British Airways – Tiketi mbili za kwenda London na kurudi.
·         Blue Bay Beach Resort, Zanzibar – nafasi ya watu wawili kwenda mapumzikoni Zanzibar kwa siku tatu pamoja na tiketi ya ndege kutoka Dar kwenda Zanzibar kwa  Zanair
·         Uhuruone – Mwaka mmoja wa kutumia bure ‘internet’ na vifaa vyake, kuvifunga na kuhudumiwa (ndani ya eneo linalopata mtandao wa Uhuruone).
·         Selous Great Water Lodge – Kifurushi cha safari fupi kwa watu wawili, pamoja na usafiri wa kutoka Dar na kurudi, kusafari kwa boti mtoni, kutembelea mbuga kwa siku nzima (na kuingia mbugani), kutembea kwa miguu msituni na kulala kwenye hoteli kubwa kwa siku mbili.
·         Coastal Travels and Sea Cliff Hotel & Spa, Zanzibar – Tiketi za kwenda Zanzibar na kurudi kwa watu wawili, pamoja na malazi ya siku mbili kwa watu wawili kwenye hoteli ya Sea Cliff Zanzibar.
·         Selous Safari Company – Malazi ya siku mbili kule Ras Kutani kwa watu wawili (vigezo kuzingatiwa).
·         Paragon Enterprises Ltd – Vocha ya dola 500 ya Tanzanite.
·         Begi la kisasa kutoka Toyota.
·         Colosseum Hotel and Fitness Club –Uanachama wa miezi miwili kwa watu wawili ama Arena Gym, Palm Residence au The Colosseum Gym.
·         Red ‘n’ White – Mfuko wa kisasa wa chapa ya Freixenet.
·         Watoto kupiga picha na Maretha L Pienaar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.