MSHAMBULIAJI Azam Fc, aliyeuzwa kwa Klabu ya Simba SC, Mrisho Ngassa, amegoma kuuzwa bila kumshirikisha katika makubailiano ya Klabu hizo mbili na kufikia muafaka kwa kufuata utaratibu.
Akihojiwa na Kituo kimaja cha Redio cha jijini Dar es Salaam jana jioni, Ngasa, alisema kuwa ameamua kutinga Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, ili kupinga kuuzwa kwake katika klabu hiyo, akitokea Azam FC bila kuhusishwa.
Akizungumzia juu ya jambo hilo, Ngassa amesema kwamba hajafanya mazungumzo ya aina yeyote na Klabu ya Simba SC wala Azam FC juu ya uhamisho wake zaidi ya kusikia taarifa za uhamisho wake katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii.
“Mimi sijui chochote, na sikatai kuhamishwa, kwa sababu mimi soka ni kazi yangu na ninaweza kucheza popote, ila taratibu zifuatwe tu, mimi si Kuku ama Samaki kwani bidhaa hiyo ndiyo inaweza kuuzwa kwa mapatano na mteja tu na mteja akachukua na kuondoka zaketu”alisema.
No comments:
Post a Comment