Habari za Punde

*NGASA AKUBALI YAISHE SASA KUVAA UZI MWEKUNDU NA MWEUPE

Baada ya mvutano baina ya Klabu ya Azam Fc, Simba na mchezaji Mrisho Ngasa, sasa Mchezaji huyo amfikia muafaka na Klabu ya Simba na kufikia makubaliano kuhusu uhamisho wake ikiwa ni pamoja na dau lake na mshahara.

Akizungumza kwenye mahojiano katika kipindi cha michezo cha Redio One, Ngasa amesema kuwa ameamua kufikia muafaka baada ya timu hiyo kufuata taratibu na kumfuata kwa mazungumzo ambapo alisema kuwa baada ya kutiliasa saini kila walichozungumza sasa yaya ni mchezaji halali wa Simba kwa msimu ujaowa Ligi Kuu.

''Sasa mimi ni mchezaji halali wa Simba ambapo sasa nitavaa jezi za rangi nyeupe na nyekundu za wekundu wa Msimbazi''. alisema Ngasa

Alipoulizwa kuhusu mapnzi yake kwa Yanga, Ngasa alisema kuwa ushabiki kwa kila mchezaji ni jambo la kawaida na yeye kazi yake ni mpira hivyo ametua Simba kufanya kazi na si ushabiki.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.