NDOTO za Simba kuvuna kitita cha Euro 600,000/= kwa kumuuza mshambuliaji wake Emaanuel Okwi kwa Klabu ya Red Bull Salzburg ya Austria, zimeyeyuka ghafla baada ya taarifa zilizoufikia mtandao huu kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda, kuwa ameshindwa majaribio yake ya kucheza soka ya kulipwa.
Habari zilizopatikana zimesema kuwa mbali na mshambuliaji huyo kukaa nchini humo kwa wiki kadhaa, akiwa katika majaribio, lakini imebainika kuwa mchezaji huyo hakuweza kukidhi mahitaji ya Klabu hiyo iliyokuwa ikimuhitaji.
Awali Viongozi wa Klabu yake ya Simba walitoa taarifa kwa wanahabari wa vyombo mbalimbali vya hapa nyumbani, wakieleza kuwa mchezaji huyo tayari alikwisha faulu majaribio yake, jambo ambalo halikuwa la kweli.
''Haikuweza kufahamika sababu zilizowafanya viongozi wa Simba kutoa taarifa za uongo, inawezekana walikuwa wakiona aibu kutoa taarifa kuwa mchezaji wao tegemezi ameferi majaribio''. alisema mtonyaji wa habari hizi
Habari kwa hisani ya Mama Pipiro
No comments:
Post a Comment