Habari za Punde

*MAONYESHO YA SARAKASI YA TIGO MAMA AFRIKA KUANZA SEPTEMBA 26, 2012

Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa Tigo Gaudence Mushi (kulia), ambao ni wadhamini wa Maonyesho ya sarakasi ya Tigo Mama Afrika akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maonyesho ya mwaka huu hayatakuwa bora zaidi ambayo pia yatakuwa ni maonyesho ya kuunga mkono sanaa na utamaduni wa Tanzania na kuwatia moyo watu wengine kufanya hivyo. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Mancom Centre, Constantine Magavilla pamoja na Ofisa habari wa Tigo Alice Maro.
 Mkurugenzi wa Mancom Centre, Constantine Magavilla (kati) akizungumza wakati wa mkutano huo. Maonyesho hayo yanayotarajia kuanza Alhamis tarehe 27 Septemba 2012 mpaka Jumapili Novemba 4, 2012 maonyesho ya sanaa ya sarakasi yatafanyika katika ukumbi wa Mancom Centre New world Cinema Mwenge, Dar es Salaam yakiambatana na programu ya nyimbo za kitamaduni na za kisasa, upindaji wa viungo, michezo ya viinimacho, michezo ya angani, michezo ya piramidi, michezo ya ufito na boriti na mingineyo mengi.
“Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa mchango wao mkubwa na kututia moyo katika maandalizi ya maonyesho haya,” alisema Constantine Magavilla Mkurugenzi wa Mancom Centre. “Tunatumaini kuwa watu hawataondoka hapa wakijisikia tu vizuri bali pia watakuwa wajumbe wazuri kwa watu wengine ili kuwashawishi wengine waje kufurahia maonyesho haya,” alisema.
 Waandishi wa habari wakionyeshwa ukumbi utakaofanyikia maonyesho hayo. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.