Habari za Punde

*ONYESHO LA TAMASHA LA JIFUNZE UTAMADUNI WA CHINA

   Wasanii kutoka nchini China wakionyesha umahiri wao wakati wa Tamasha la  Jifunze  Utamaduni wa  China lililofanyika jana jijini Dar es Salaam, ambao makundi mbalimbali ya china yalitoa burudani za aina mbalimbali ya michezo jukwaani.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (kulia) akikaribishwa na Balozi wa China  nchini Tanzania  Lu Youqing (kushoto) allipohudhuria hafla ya Tamsaha la  Jifunze  Utamaduni wa  China lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizra ya Nishati na Madini Eliakim Maswi,  akitoa hotuba yake wakati wa  onyesho la tamasha la jifunze utamaduni wa China katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijijni Dar es Salaam, ambapo aina za michezo mbalimbali  pamoja na nyimbo, mazingaombwe kutoka kikundi cha Utamaduni cha Taifa kutoka China kilionyesha na kutoa burudani safi  kwa wageni waliohusduria,
 Mmoja wa wanavikundi wa China akitoa b urudani.
Kikundi cha Utamaduni cha Taifa kutoka China kikionyesha sanaa yao jukwaani. 
 Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia tamasha hilo.
Kikundi cha utamaduni  kutoka Tanzania kikitoa burudani, jukwaani. Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.