NA MAGRETH KINABO-MAELEZO SERIKALI iko katika mchakato wa kuanzisha Benki ya Vijana ili waweze kukopeshwa na kujiletea maendeleo. Kauli hiyo imetolewa leo (jana) na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala wakati akifungua warsha ya siku mbili ya Uratibu wa Maendeleo ya Sekta ya Vijana inayoendelea katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, iliyoandaliwa na Shirika la Restless Development, kwa niaba ya Waziri husika, Dk. Fenella Mukangara. “Wizara tayari imeanza mchakato wa kuanzisha Benki ya Vijana ambayo riba yke itakuwa nafuu kama ilivyo Benki ya Wanawake. Tutaomba fedha katika bajeti ya mwaka ujao wa ili kuianzisha,” alisema Waziri Makala. Alisema vijana pia watapewa elimu ya namna ya kuweza kukopa na kurejesha , ambapo mafunzo hayo yatafanyika Kilosa na Marangu. Aliongeza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya Mfuko wa Vijana kukopesha sh. bilioni 1.2, lakini fedha zilizorudishwa ni sh. milioni 60 tu. Waziri Makala aliwataka vijana kuacha tabia ya kulalamika badala yake wafanye kazi na kutengeneza taifa lenye migogoro ya maendeleo kwa kuwa suala la maendeleo ya taifa liko mikononi mwao. Akizungumzia kuhusu suala la ukosefu wa ajira aliwasisitizia kuwa halitatuliwa la serikali pekee, bali linahitaji ushirikiano wa pande zote zikiwe fursa za kujiari wenyewe. Aidha aliwataka vijana hao kutoa maoni juu ya uundaji wa katiba kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo yanayohusu vijana bila kushawishiwa viongozi wa kisiasa dini, mashirika na taasisi. |
MERIDIANBET YASHUSHA TABASAMU ALI MAUA
-
Mabingwa wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet wameendelea
kuhakikisha wanasaidia na kurudisha tabasamu kwa jamii kwa ambavyo
wamefanya leo mae...
54 minutes ago
No comments:
Post a Comment