Habari za Punde

*YANGA YAZINDUKA BILA KOCHA YAICHAPA JKT RUVU 4-1 IKIWA NA MINZIRO

 Kikosi cha Yanga.
 TIMU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, leo imefuta machungu iliyoapata katika mechi zake mbili za awali za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuichapa JKT Ruvu kwa jumla ya mabao 4-1 katika mchezo uliochezwa leo jioni katika uwanja Taifa.

.Katika michezo yake miwili ya awali timu hiyo ilitoka sare ya 0-0 na Prisons ya jijini Mbeya na katika mechi yake ya pili Yanga ilikubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar.
Baada ya matokeo mabaya ya michezo hiyo miwili Klabu hiyo siku ya Jumamosi ilitangaza rasmi kumtimua kocha wao Mbelgiji Tom Saintfiet na kumkabidhi mikoba kocha wake msaidizi Fredy Minziro ambaye leo ameiongoza vyema timu hiyo na hatimaye kuibuka na ushindi mnono.
Bao la kwanza la Yanga limefungwa na beki mahiri Nadir Haroub 'Canavaro' katika dakika ya 4, bao la pili na la tatu limefungwa na shambuliaji mpya, Didier Kavumbagu, aliyejiunga na Yanga katika kipindi kilichoisha cha usajili akitokea katika klabu ya Atletico ya Burundi, katika dakika ya 31 na 65,.
Bao la nne limewekwa kimiani na Simon Msuva katika dakika ya 52 na bao la JKT Ruvu limefungwa na Credo Mwaipopo.
Kavumbagu ambaye alianzishwa kwa mara ya kwanza leo baada ya mechi zilizotangulia kuingia kutokea benchi na kuonekana hatari kwa mashuti yake makali, alifungua akaunti yake ya maagoli kwa klabu yake mpya huku mengine mawili yakifungwa na Simon Msuva na beki Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Ushindi huo umeifanya Yanga, ambayo iliingia uwanjani leo ikiwa katika nafasi ya 13 katika msimamo wa timu 14 kutokana na kuwa na pointi moja, kufikisha pointi nne.
Washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam walikwea kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha pointi 7 kufuatia ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Chamazi katika mechi nyingine iliyochezwa leo. Goli la Azam lilifungwa na Kipre Tchetche.
Mabingwa Simba wenye pointi 6 kutokana na mechi mbili watacheza kesho kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya Ruvu Shooting.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.