Benki ya Barclays Tanzania
imetangaza kuongeza muda wa kampeni yake ya Amana za Muda Maalumu hadi Desemba
31 Mwaka huu. Kampeni hii ilizinduliwa rasmi Agosti 6, 2012 na ilikuwa ifikie
mwisho wake Desemba 6 Mwaka huu. Wateja wa Barclays wa Kitengo cha Kibenki cha
akaunti binafsi kama vile Wateja Binafsi,
Wateja Wakubwa na Wafanyabiashara wanaweza kufurahia faida ya kuweka Amana za
Muda Maalumu na Barclays.
Kampeni
hii imetengenezwa kupitia bidhaa ya kipekee ya Barclays inayofahamika kama ‘Regular Interest Fixed Deposit’. Mteja anayefungua
Akaunti ya Amana ya Muda Maalumu yenye Faida ya Kawaida ataweza kulipwa faida ya
amana yake kila mwezi kwa kipindi chote cha muda wa amana yake tofauti na
ilivyo kwamba faida hutolewa tu mwishoni mwa kipindi cha akaunti hiyo maalumu.
“Kiwango
cha chini ambacho wateja wanatakiwa kuwa nacho ni shs milioni 15 na muda wa
chini ambao amana hiyo itatakiwa kuwemo katika akaunti ya Barclays ni mwaka
mmoja na muda wa juu ni miaka 5,” alisema Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa
Barclays, Samwel Mkuyu.
Bwana
Mkuyu aliongeza kwa kusema: “Faida ya kila mwezi kwa wateja italipwa kwenye
akaunti zao za kawaida na faida kwenye fedha ya msingi iliyowekwa kwenye
akaunti ya Muda Maalumu itatolewa mwishoni mwa kipindi husika. Tuna aina tofauti kwa viwango tofauti na
maelezo yake kwa kina yanapatikana kwenye matawi yetu yote nchini Tanzania.
”
Aliendelea:
“Sisi Barclays, tumedhamiria kuifanya sekta ya benki Tanzania kuwa rahisi zaidi kwa
wateja wetu kwa kuleta huduma rahisi zinazopatikana kwa wote. Wateja wetu
wataendelea kufurahia huduma za bure za kidijitali ikiwa ni pamoja na kutoa
fedha bure kwenye mashine za ATM, huduma ya bure ya ujumbe mfupi kupitia simu
za mkononi, kupata taarifa za akaunti bure kupitia mtandao na huduma za kibenki
kupitia mtandao wa intaneti”.
Kwa taarifa zaidi wasiliana
na:
Tunu
Towo Kavishe
Mkuu
wa Mahusiano na Mawasiliano
+255
228 2018
Barclays
Bank Tanzania
About
Barclays
Barclays is a major global financial services provider
engaged in personal banking, credit cards, corporate and investment banking,
and wealth and investment management. With over 300 years of history and
expertise in banking, Barclays operates in over 50 countries and employs
approximately 140,000 people. Barclays moves, lends, invests and protects money
for customers and clients worldwide. For more information, please visit the
Barclays website: www.barclays.com
About
Barclays in Africa
The businesses in scope for the proposed combination
employ more than 8,000 people and have a network of more than 400 branches and
750 ATMs serving approximately 2.2 million customers. As at December 2011, the Barclays Africa
businesses in scope for the proposed combination had total assets of
approximately GBP6 billion.
About
Barclays Tanzania
Barclays Bank Tanzania Limited first opened its doors
in Tanzania in 1925 and
continued to operate in the country until 1967 when its Tanzania
operations were nationalized to become National Bank of Commerce. With the
liberalization of the economy in 1990s, Barclays Bank Plc made a decision to
re-enter the Tanzania
market and re-opened its doors in the year 2000. Barclays Bank Tanzania now
has 22 branches, 41 ATMs strategically located countrywide, over 400 employees
and over 110,000 customers.
No comments:
Post a Comment