Na Mwandishi Wetu
WASHIRIKI wa fainali za taifa za urembo mwaka huu 'Redd's Miss Tanzania 2012' wametakiwa kuwa na nidhamu wakati wote watakapokuwa kambini wakijiandaa na shindano hilo litakalofanyika mapema mwezi ujao hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na warembo hao jana baada ya kuwasili kambini, Mratibu wa shindano hilo, Hashim Lundenga, aliwaambia washiriki hao kuwa kila mmoja anawajibika kumuheshimu mwenzake na hakuna aliye na thamani kubwa kulimo mwingine.
Lundenga aliwaambia warembo hao wawe wanajitambua na hilo litawajenga katika maisha yao na kuwatakia waishi kwa furaha katika muda wote watakaokuwa kwenye kambi hiyo.
"Karibuni wote hapa kwenye hoteli hii ambayo itakuwa ndio makazi yenu katika kuelekea shindano la Redd's Miss Tanzania, ila wanaambia kwamba wote mko sawa na kikubwa ni kuwa na nidhamu," alisisitiza mratibu huyo.
Aliwaambia warembo hao kwamba wakiwa kwenye kambi hiyo watafundishwa mambo mbalimbali yanayohusiana na sanaa ya urembo, kujiandaa na maisha na kujitambua.
Aliwataja warembo hao waliongia kambini jana kuwa ni pamoja na Noela Michael, Magdalena Roy, Mary Chizi, Naombi Jones, Carren Elias, Venancy Edward, Warid Frank, Anande Raphaely, Lucy Stephano, Rose Lucas, Irene Veda, Joyce Baluhi, Virginia Mokiri, Fatma Twahil, Phina Revocatus, Belinda Mbogo, Lightness Michael, Elizabeth Diamond, Bridgitte Alfred, Diana Hussein na Irene David.
Aliwataja washiriki wengine kuwa ni Zuwena Nassib, Edda Sylivester, Flavia Maeda, Catherine Masumbigana, Jesca Haule, Eugene Fabian, Happiness Daniel, Happiness Rweyemamu na Babylove Kalalaa.
Mrembo anayeshikilia taji la mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Nchini (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's ni Salha Israel aliyetokea Kanda ya Ilala hapa jijini.
|
Kauli ya Serikali kuhusu Chuo cha Kodi, 400 wahitimu “Inasaidia kuongeza
makusanyo”
-
Serikali kupitia Wizara ya Fedha imesema mchango wa Chuo cha Kodi unasaidia
kuongeza makusanyo ya Mapato ya Serikali na kuleta uhalisia wa kiutendaji.
“S...
5 hours ago
No comments:
Post a Comment