Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa mfanyakazi katika
Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, Jenkins Chochole Matulile, aliyefariki
dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu
zilifanyika nyumbani kwao Mbezi Tangi
Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji
Mama Mzazi wa marehemu, Jenkins Chochole Matulile, wakati alipofika
nyumbani kutoa pole na heshima za mwisho
kutokana na msiba huo wa aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar
es Salaam, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za
kuaga mwili wa marehemu zilifnyika nyumbani kwa kwao Mbezi Tangi Bovu na
kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na
mkewe, Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili
wa marehemu, Jenkins Chochole Matulile, aliyekuwa
mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, aliyefariki dunia
mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika
nyumbani kwao Mbezi Tangi Bovu na
kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam leo.
Makamu akijumuika na waombolezaji.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba huo.
No comments:
Post a Comment