Habari za Punde

*MAMA MLALA NJE ASAKA WAFADHILI KUWAPELEKA WATOTO WAKE SHULE MWAKANI

Ili kuonyesha nia ya kutaka watoto wake sita waweze kusoma na kufikia hatua nzuri ya kupata elimu ya Juu, tayari Mama huyu, ambaye jina halisi ni Agness King'ombe, ambaye alibadili dini na kuitwa jina la kiislam, Sada Masoud, anayewaacha watu wengi na maswali yasiyokuwa na majibu pindi wanapomuona akiwa katika maeneo yake ya makazi eneo ya Ufukwe wa bahari ya Hindi pande za Ocean Road, amekwishaanza kuwafundisha na kuwapa elimu ya awali watoto wake wa5, wenye umri wa kuanza masomo ya darasa la kwanza huku mtoto wake wa kwanza mwenye umri wa miaka 12, Dyana Sailas, alitakuwa kuwa darasa la Sita kwa sasa.

Je, wajua ni kwa nini Mama huyu alibadili dini na kuwa Muislam na kutumia jina hilo la Sada? kaa nami, katika ukurasa huu.
Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Sada, alisema kuwa, maisha anayoishi si kwamba anapenda kuishi katika staili hiyo, la hasha, bali ni sehemu tu ya maisha na staili ya masiha ya kiafrika iliyompelekea kuwa katika hali hiyo na kujikuta kila mtoto anakuwa na baba yake.

Aidha, sada alisema kuwa amekuwa akipata msaada wa kuwalea watoto wake kutoka kwa baadhi ya baba wa watoto wake wanaomkumbuka siku moja moja, na kuamua kutumia sehemu ya msaada huo kuwanunulia watoto chakula, nguo na vifaa vya kuwafundishia watoto hao iki ni pamoja na Unifomu, Ubao, chaki, Vitabu na madaftari.

''Nimeamua kuwaandaa watoto wangu kwa kuwafundisha kusoma na kuandika, na pia nawafundisha masomo ya Kiswaahili, Kiingereza na Hesabu, ili kuwaandaa waweze kujua vyema ili atakapojitokeza mfadhili wa kunisaidia niweze kuwapeleka kuanza shule mwakani, na naamini hata walimu hawatapata shida katika kuanza nao kwani tayari wanaweza kusoma na kuandika vizuri tu,

Huyu wa kwanza Dyana, kwa sasa alitakiwa awe tayari yupo darasa la Sita lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu, nilishindwa kumpeleka kuanza shule hadi sasa, lakini si haba nikipata mfadhili hata naye pia itabidi aanze tu la kwanza''. alisema Sada.

Akielezea staili ya maisha yake katika eneo hilo, sada alisema kuwa ikitokea siku amebahatika kupata fedha za kutosha hujitahidi kukodi Hoteli ya bei nafuu na kulala na watoto wake, na pindi anapokosa huwa tayari ameshajiandaa ambapo hutumia Hema maalum ambalo hulijenga nyuma ya Hoteli ya Serena na kutumia magodoro ya kujaza na kufunga Neti kubwa na kisha kuuchapa usingizi na wanawe na kisha kuondoa asubuhi.

''Nimeamua kuchagua eneo hili la chini ya mti kuwa makazi yangu na kama ofisi yangu nikiwa kama mwalimu wa watoto wangu na pia nikiwa kama mfanyakazi wa watoto wangu, kwa sababu eneo hili wanangu hupata maji kwa urahisi tu hapoa Gymkhana kwa ajili ya kuwafulia nguo zao na kuwapikia chai ili wanywe kabla ya kuanza vipindi kuwafundisha.

Na ninapofika hapa asubuhi baada ya kuamka, kuwaandalia chai kwanza wanangu na kuwaogesha na kuwavisha Unifom na baada ya kunywa chai hukaa kama hivyo kwenye mkeka kama unavyowaona wakinisubiri nimalize kazi zangu ili tuanze darasa''. alisema Sada

ZIJUE SABABU ZA MAMA HUYU KUBADILI DINI
''Sababu za mimi kubadili dini ni kwamba, hivi sasa nina watoto Sita, ambao kila mmoja ana baba yake, na baba mmoja kati ya hao sita alinidanganya nibadili dini ili aweze kunioa na tuishi pamoja, lakini mwisho wa siku akanitelekeza na kunikimbia hadi leo sijawahi kumuona tena baada ya kuniachaia mtoto''. alisema Sada

Sada aliwataja kwa majina watoto wake kuwa ni, Dyana Silas, Michael Willson, Junior Jonathan, Godlisa Carlos, Gudluck Alex na Trywell Jumpo, ambao wote anaishi nao katika mazingira hayo magumu.
 Watoto wa Bi. Sada, wakiwa darasani wakimsubiri mwalimu Mama yao kuanza kuwafundisha leo asubuhi, huku wakiwa katika sare za shule.
 Bi Sada, akiwa bize kumalizia kazi zake za kuosha vyombo baada ya kumaliza kunywa chai na kuwaogesha watoto, wake ambao ni wanafunzi wake pia.
 Wanafunzi hao wakijisomea, wakati wakimsubiri mwalimu wao...(kushoto) ni mtoto wake mdogo yeye akicheza tu...
Wanafunzi hao wakijisomea, wakati wakimsubiri mwalimu wao...
Hii ni sehemu ya kwanza, endelea kufuatilia mahojiano haya katika mtandao huu wiki ijayo, Sababu za kuachwa na kila mwanaume.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.