Habari za Punde

*PUSH MOBILE YAMZAWADIA MSHINDI WA SERENGETI FIESTA 2012 MAGARI MAWILI

 Meneja Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rugambo Rodney (kushoto) akimkabidhi funguo za magari mawili, Diana Elis Mkoba, baada ya kushinda shindano la Tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Diana alikabidhiwa magari mawili aina ya Vitz yenye thamani ya shs milioni 18.Katikati ni Baba mdogo wa mshindi, Gratian Mkoba ambaye ni Rais wa chama cha Walimu Tanzania (CWT).
Mshindi wa magari mawili yaliyotolewa na kampumi ya Push Mobile kwa ajili ya tamasha la Serengeti Fiesta, Diana Elis  Mkoba, akiwa ndani ya moja ya gari alizozawadiwa baada ya kushinda bahati nasibu hiyo. Picha na Mpiga Picha Wetu
******************************************
 Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Push Mobile imemkabidhi, Diana Elisa Mkoba,  Magari mawili aina ya  Vitz  yenye thamani ya sh. million 16 kufuatia promosheni iliyoendeshwa wakati wa tamasha la Fiesta katika mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara.
Magari hayo yalikabidhiwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rodney Rugambo katika hafla fupi iliyofanyika jijini, Dar es Salaam leo.
Rugambo alisema kuwa wamefarijika kuwa wadhamini wasaidizi wa tamasha hilo lililodhaminiwa na bia ya Serengeti kutokana na kutoa mchango wao katika jamii, hasa kwa kupitia muziki wa kizazi kipya.
Alisema kuwa zawadi hiyo ya magari mawili ni itimisho la magari sita waliyotoa katika mikoa mbali mbali wakati wa tamasha hilo. Kampuni hiyo ilitoa gari moja moja mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza na Dodoma.
Mbali ya zawadi hizo, kampuni hiyo pia ilitoa zawadi ya pikipiki 15, simu ya mkononi aina ya Nokia dabodabo 130, simu aina ya blackbey 14 na washindi wa fedha taslim shs milioni 20. Thamani ya vitu vyote hivyo ni milioni 200.
“Ni matarajio yetu kuwa Diana atayatumia magari haya ipasavyo na tunampongeza kwa ushindi, watu wengi walishiriki katika bahati nasibu hii na Diana kubahatika kushinda magari mawili, tunawaomba wadau washiriki katika promosheni zetu nyingine,” alisema Rodney.
Diana alisema kuwa amefurahi kushinda zawadi hiyo kwani hakuamini baada ya kupokea simu ya ushindi wa zawadi hizo.  Alisema kuwa kwa vile yeye ni mwanafunzi wa chuo cha Bandari atatumia gari moja na lingine atajua wapi kulipeleka, kama Kagera kwa mama yake au libaki hapa hapa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.