Habari za Punde

*WAHUDUMU WA BAA KUNOLEWA JINSI YA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA WAO DAR, NAIROBI


Wahudumu mbalimbali wa Baa nchini, leo watapata mafunzo maalum ya jinsi ya kuwahudumia wateja wanaotumia pombe kali (whiski) kutoka kwa balozi wa kinywaji cha Glenmorangie, Niel Hendriksz.
Mafunzo hayo yanalenga kutoa upatikanaji wa huduma bora sambamba na uchanganyaji wa kinywaji hicho kwa lengo la kuwafanya wanywaji kupata kinywaji kilicho bora kwa afya zao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Hendriksz ambaye  yuko nchini kwa ziara ya siku mbili alisema kuwa, wameamua kufanya mafunzo hayo ili kuboresha huduma zao ikiwa ni njia moja ya kuboresha soko la kinywaji hicho hapa nchini.
Aidha alisema kuwa, bidhaa zao zinatengenezwa nchini Scotland, na wamedumu kwa kipindi kirefu katika soko na sasa wameamua kuongeza nguvu kwa upande wa huduma.
Mbali na kutoa mafunzo hayo, barozi huyo atawaelimisha wahudumu hao juu ya uelewa kuhusu utumiaji wa vinywaji hivyo katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema kuwa kwenye ziara ya siku tano  katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo hapa nchini atakuwapo kwa siku mbili na mafunzo mengine atayatoa nchi nyingine.
Alifafanua kuwa atakutana na makundi tofauti ya utoaji wa huduma ya kinywaji chao mbali ya wafanya biashara mbali mbali kwa lengo la kudumisha soko.
“Kutakuwa na nafasi 20 kwa nchi nzima kuhudhuria mafunzo ambapo pia tutabadilishana mawazo na watu mbali mbali ambao ni wadau wa kinywaji chetu," alisema.
 Ziara ya  Hendrisksz inatarajia kumalizika  keshokutwa ambapo ataelekea jijini Nairobi, Kenya kwa mwendelezo wa ziara hiyo Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.