WAZIRI WA UJENZI, MH. DR. JOHN POMBE MAGUFULI (MB) ATAWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO KWA AJILI YA KUPANGISHA OFISI LINALOJENGWA NA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA MKOANI DODOMA.

Sherehe za uwekaji jiwe la msingi zitafanyika eneo la Mpwapwa Flats, Mtaa wa Moshi kuanzia saa mbili asubuhi.
Viongozi wa Serikali Mkoani Dodoma pamoja na Taasisi mbali mbali pia watashiriki katika sherehe hizo.
Mradi huu wa jengo la ofisi ni mwendelezo wa azma ya Serikali kupitia Wakala wa Majengo nchini wa kujenga majengo kwa ajili ya kupangishia shughuli za ofisi.
Taarifa hii imetolewa na;- Balozi Herbert Mrango
No comments:
Post a Comment