Kiungo wa Timu ya Yanga, Haroun Niyonzima (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Simba, Shomari Kapombe, katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliochezwa jana katika uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Beki wa kushoto wa Yanga, Stepano Mwasika, akimdihibiti beki wa kulia wa Simba, Nassor Masoud 'Cholo', wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
*****************************************
*Katika dakika ya 77, mwamuzi, Mathew Amkrama, alimtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja Simon Beki wa Yanga,
Na Mwandishi Wetu
WATANI wa jadi, Yanga na Simba wametoka sare ya bao 1-1 katika mchezo ambao ulishuhudia maamuzi ya kutatanisha kutoka kwa waamuzi wa mechi hiyo.
Pamoja na tambo, utani na masihara kadhaa, maelfu wa mashabiki walioshuhudia mchezo wenye upinzani wa kila aina huku Mbuyu Twite, Kelvin Yondani na Mrisho Ngassa wakiwa ndiyo gumza kabla na baada ya mechi hiyo.
Simba SC walianza mchezo kwa kasi na kufanya mashambulizi mawili ya haraka haraka katika daika ya kwanza nay a pili, hata hivyo kipa wa Yanga, Yaw Berko aliokoa hatari zote. Simba SC iliendelea kuishambulia Yanga na kupata bao la kuongoza katika dakika ya nne kupitia Amri Kiemba kufuatia pasi nzuri ya Mwinyi Kazimoto kutoka wingi ya kulia.
Beki wa Yanga, Stephano Mwasika alifanya kosa kwa kwenda kugombea mpira wa kurusha na Cholo akauwahi na kumrushia Felix Sunzu aliyemwekea Kazimoto na Kiemba kufunga kirahisi huku beki ya Yanga ikishangaa kikanchoendelea.
Baada ya bao hilo, Simba iliendelea kusukuma mashambulizi na mabeki wa Yanga wakiwa wanafanya kazi kubwa ya kuokoa. Yanga ilibadili kibao katika dakika ya 16 na kuanza kufanya mashambulizi mfululizo, na kama si utani wa Simon Msuva na Hamis Kiiza, timu hiyo ingeweza kusawazisha bao hilo dakika ya 28.
Baada ya kuona kuwa Kiiza hayupo ‘serious’, kocha mkuu wa Yanga, Ernie Brandts alimtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Frank Dumayo, ambaye alibadili mchezo huo na shutila Twite kugonga mwamba wa juu dakika ya 38 huku Kaseja akiwa hajui la kufanya.
Yanga iliendelea kutawala kwa kasi kuwafanya Simba kuweka mikakati mingi kipindi cha pili na kuchelewa kutoka vyumbani kwa dakika nane. Hali hiyo ilisababisha mechi hiyo kuchelewa.
Watoto wa Jangwani waliingia kipindi cha pili kwa kasi kubwa na hasa baada ya kuingia kwa Didier Kavumbagu baadala ya Nizar Khalfan. Timu hiyo ilifunga bao dakika ya 61 kupitia kwa Kavumbagu, pamoja na mwamuzi kuashiria mpira kuwekwa kati, Kaseja alijiangusha na mwamuzi kubadili maamuzi yake.
Yanga iliendelea kuliandama lango la Simba na kulazimisha kocha wake, Cirkovic Milovan kumtoa Edrward Christopher na nafasi yake kuchukuliwa na Daniel Akuffor, hata hivyo mabadiliko hayo hayakuwasaidia na Yanga kusawazisha kupitia kwa Saidi Bahanuzi kwa njia ya penati baada ya beki Jonas Mkude kuunawa mpira wa kurusha wa Mbuyu Twite.
Baada ya bao hilo, Simba ilibadili mchezo na kufanya mashambulizi kupitia kwa Ngasa, hata hivyo Berko alikuwa makini na kuosha hatari zote. Yanga ilipata pigo dakika ya 77 baada ya Simon Msuva kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kurudishia rafu kwa Juma Nyoso. Pamoja na kadi hiyo, Yanga iliendelea kukosa mabao kupitia kwa Kavumbagu (mabao mawili) huku Kaseja akifanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Bahanuzi katika dakika ya mwisho ya nyongeza.
katika mechi ya timu hizo za U- 20, Simba iliponea chupuchupu baada ya kusawazisha mabao mawili wakati mechi ikiwa imebakia dakika tatu. Mabingwa hao wa BancABC walishindwa kuonyesha cheche kwa Yanga ambao wameisuka timu yao ipasavyo.
*VITUKO KABLA YA MECHI
Yanga walikuwa wa kwanza kuingia uwanja wa Taifa mafira ya saa 10.59 wakiwa na basi lao jipya na aiyefungua dimba la kukanyaga ardhi ya uwanja huo alikuwa Nadir “Cannavaro” Haroub na kufuatiwa na Hamis Kiiza, Yaw Berko na wengine.
Uingiaji huo ulikuwa na mikwala mingi huku baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wakiwafukuza baadhi ya watu wasiojulikana ni wa upande gani. Wanachama maarufu wa Yanga, Mustapha, Saidi Motisha na Bakili Makele walikuwa makini katika zoezi hili na kuhakikisha kuwa kila waliochopewa maagizo kinafuatwa.
Ndani ya kuingilia vyumba vya kubadilishia, kulikuwa na ulinzi mkali na kila anayeingia alikaguliwa ili kuondoa hujuma. Yanga pia wakawa wa kwanza kuingia uwanjani kwa ajili ya kupasha viungo moto.
Kama ilivyokuwa kwa Yanga, Simba nao waliingia uwanjani saa 11.13 na ulinzi ulikuwa mkali huku Juma Kaseja akiongoza jahazi. Timu hiyo pia ilikuwa ya pili kuingia uwanjani kupasha miili moto. Yanga pia ilikuwa ya kwanza kutoka uwanjani baada ya kipindi cha kwanza nay a kwanza kuingia kuanza kipindi cha pili.
Simba ilichelewa kuingia kipindii cha pili kwa dakika nane(8) na kuonywa na mwamuzi kwani walichelewesha matangazo ya ‘live’ ya kituo cha televisheni cha SuperSport.
VITUKO KAMILI VYA MECHI HIYO NA MADUDU YA WAAMUZI FUATILIA BAADAYE..........
No comments:
Post a Comment