Baadhi ya wachezaji wa Yanga, wakishangili moja kati ya mabao yao mawili walioifunga Azam, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Jana Yanga iliichapa Azam kwa mabao 2-0, ambapo Yanga sasa imeiondoa Simba kileleni baada ya kufikisha jumla ya Pointi 26, huku ikiwa imesalia na mchezo mmoja mkononi na Coast Union ya Tanga ili kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi hiyo.
Akizungumza na mtandao huu Nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' alisema kuwa kipigo hicho ni maalum kwa ajili ya kumkaribisha Kocha wa timu hiyo,Stewart Hall, ambaye aliwahi kutimuliwa na timu hiyo na kisha wakamrejesha baada ya kocha mpya aliyekuja kurithi mikoba ya Stewart,Boris Bunjak, kutimuliwa tena wakati timu hiyo ilipokubari kipigo cha mabao 3-1 na Simba.
''Sasa tunataka tuone Azam watamtimua tena Kocha Stewart au wataanza kutimua wachezaji, Soka la Bongo hatuchelewi kuanza kutafutana uchawi baada ya kufungwa, inabidi wakubali tu matokeo kuwa tuliwazidi kila idara kimchezo na ndiyo maana tumefunga, ila mimi nilikuwa nilivyokuwa nataka ndivyo imekuwa ili hao viongozi waone kuwa kufukuza kocha sio suluhisho ila ni kukubali na kujipanga waone walipokosea''. alisema Nadir
Simon Msuva (kushoto) akimenyana na Said Mora, wakati wa mchezo huo.
Kavumbangu, (juu) akitupia bao, wakati wa mchezo huo.
Wachezaji wa Yanga, wakishangili na kumpongeza Kavumbangu.
No comments:
Post a Comment