Redd's Miss Sinza, Redd's Miss Kinondoni na Redd's Miss Tanzania 2012, Bridgit Alfred (katakati) akipunga mkono kwa furahaa baada ya kutangazwa kuibuka mshindi na kuvishwa Taji hilo katika shindano la Taifa lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Ubingo Plaza, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa Pili,Eugene Fabian. Akizungumza na mtandao huu ambao pia ulikuwa ni miongoni mwa wadhamini wa Shindano la Miss Sinza 2012, shindano lililofanikisha kumpata Miss Kinondoni na hatimaye Miss Tanzania, 2012, mwandaaji huyo Majuto Omary, alisema kuwa amefarijika sana kuona kwa mara ya kwanza Kitongoji chake cha Sinza kimefanikiwa kutoa Miss Tanzania ambaye pia alikuwa ni chaguo la wengi na wadau wa fani hiyo ya urembo.
Aidha Majuto, alisema kuwa baada ya kusikia jina la mrembo wake likitangazwa na mtangazaji Tom Chilala, ambaye alikuwa akisema kuwa mrembo huyo ni faraja kwa waandishi wote wa habari kutokana na kutokea katika Kitongoji na mwandaaji ambaye ni Mwanahabari, alifarijika sana na kusema kuwa hivi sasa ameanza maandalizi ya kumuandalia Party Mrembo huyo ili kumpongeza kwa kutwaa taji hilo.
Majuto alisema kuwa anatarajia kutoa Taarifa kwa wanahabari hii leo kuhusiana na maandalizi ya mnuso huo ambapo anatarajia kuweka wazi siku na mahala itakapofanyika hafla hiyo, pamoja na burudani.
Redd's Miss Sinza, Redd's Miss Kinondoni na Redd's Miss Tanzania 2012, Bridgit Alfred (katakati) akiwa na washindi wenzake, mshindi wa pili Eugene Fabian (kushoto) na Mshindi wa Tatu,Edda
Sylvester.
Washiriki wakicheza shoo ya pamoja ya ufunguzi.
Sehemu ya waandishi wa habari wadau wa urembo, wakiwa ukumbini hapo wakati wa shindano hilo.
Shoo ya ufunguzi...
Sehemu ya wadau na mashabiki wa fani ya urembo....
Baadhi ya warembo wa miaka iliyopita, Faraja Kotta na Flaviana Matata, wakipozi na warembo wenzao.
No comments:
Post a Comment