Habari za Punde

*AJALI KATIKATI YA MJI YAJERUHI

 Gari aina ya Toyota Crisser, likiwa limelala ubavu baada ya kugongana na gari aina ya Harier, katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, eneo la Red Cross, juzi Jumamosi. Haikuweza kufahamika mapema chanzo cha ajali hiyo, ambayo ilisababisha dereva wa gari hii iliyolala ubavu, ambaye hakuweza pia kufahamika jina lake, kupata majeraha kadhaa usoni.
 Dereva wa gari lililopinduka, akiwa na majeraha usoni baada ya kutoka katika gari lake hilo lililoanguka mbele kabisa ya Kituo cha Daladala cha Red Cross.
 Dereva huyo, akiangalia gari lake wakati akisubiri taratibu za kufika kwa askari wa usalama barabarani ili kupima ajali hiyo.
Gari lililohusika na ajali hiyo, lenyewe likiwa limeharibika Shoo ya mbele tu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.