(A)
Msama yapiga jeki mkutano
TASWA
KAMPUNI ya Msama Promotions
inayoandaa Tamasha la Pasaka imeahidi kutoa Sh. Milioni 1.5 kwa ajili ya Mkutano
Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika
Bagamoyo mkoani Pwani wiki ijayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi
ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ndiye Mkurugenzi wa kampuni hiyo amesema
ushirikiano wake na wanahabari umemsukuma kusaidia kiasi hicho cha
fedha.
Msama
ameahidi kuendelea kushirikiana na TASWA kadri awezavyo na kwamba mafanikio ya
Tamasha la Pasaka yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na wanahabari.
Kampuni yangu ya Msama Promotions
kupitia Tamasha la Pasaka tumeamua kuungana na wanahabari katika kufanikisha
mkutano wenu, tunaamini uhusiano wetu utaendelea kuwa wa kupigiwa mfano,”
ilisema sehemu ya taarifa ya TASWA jana ikimkariri Msama.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando alishukuru kwa udhamini huo na
kuomba wengine wenye moyo wajitokeze kuwasaidia kwani bajeti yao ni Sh. Milioni
20. Tayari kampuni ya simu za mkononi ya Zantel imeshatangaza udhamini wa Sh.
Milioni sita.
Mhando
alisema maandalizi ya Mkutano Mkuu wa TASWA utakaofanyika wiki ijayo Bagamoyo
mkoani Pwani yanaendelea vizuri na kwamba zaidi ya wanachama 100 wa TASWA na
wadau wengine wa TASWA wamethibitisha kushiriki.
(B)
Pongezi
Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kinatoa pongezi kwa wanachama
wake Benny Kisaka na Zena Chande kwa kufanikiwa kuwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kisaka
alishinda wadhida huo wiki iliyopita kupitia uchaguzi wa Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), wakati Chande alishika Jumatano katika
uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA).
Tunaamini
wajumbe wa Mkutano Mkuu DRFA na wale wa TWFA hawakufanya makosa, wamefanya
uamuzi sahihi na wamepata watu sahihi na makini na michango yao itakuwa yenye
tija kubwa kwa maendeleo la mpira wa miguu hapa nchini.
Tunawatakia
kila la heri wanachama wetu hao katika changamoto mbalimbali watakazokutana nazo
kwenye nafasi zao hizo walizopata.
Amir
Mhando
Katibu Mkuu
TASWA
20/12/2012
No comments:
Post a Comment