BAN KI MOON ATAKA MTIZAMO MBADALA KATIKA KUISAIDIA DRC
Na Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema , katika siku tano zilizopitaamekuwa akifanya mazungumzo kwa njia ya simu na baadhi ya viongozi waAfrika, mazungumzo yaliyokuwa na lengo la kuwa na mpango mpana wakisiasa utakaoweza kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Marais wa Afrika ambao Ban Ki Moon amewataja kwamba amefanya naomazungumzo kwa njia hiyo ya simu ni pamoja na Rais wa Tanzania, Mhe, Jakaya Mrisho Kikwete.Marais wengine ni wa Afrika ya Kusini, Angola, Uganda, Rwanda, Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo na Rais wa Jamhuri ya Kongo.
" Labda niwaeleze hili, siku tano zilizopita na hata mwishoni mwa wikinimekuwa nikifanya mawasiliano kwa njia ya simu na viongozi kadhaa waAfrika, kwa lengo la kuangalia kama tunaweza kuwa na mpango mpana wakisiasa utakaosaidia kufikia uamuzi wa haraka kuhusu hali ya Mashariki yaDRC.
Na leo mchana nitafanya mazugumzo pia na Mwenyekiti wa Kamisheniya Umoja wa Afrika, Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma" akaeleza Ban Ki MoonMkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, ameyabainisha hayo wakati alipokuwaakijibu maswali ya waandishi wa habari ambao pamoja na mambo menginewalitaka kufahamu kilichokuwa kikiendelea DRC na suala la ukiukwaji wahaki za binadamu katika eneo la Mashariki ya nchi hiyo.
Ban Ki Moon alikutana na kufanya mazugumzo ya mwisho wa mwaka naKlabu ya Waandishi wa Habari wa Umoja wa Mataifa, mkutano huo ambaoulifanyika siku ya jumatano aliutumia kuainisha masuala mbalimbaliyaliyojiri katika mwaka huu unaomalizika likiwamo suala la DRC.
Pamoja na kufanya mawasiliano ya simu na viongozi hao waafrika na kutakakujua mawazo yao na maoni yao kuhusu mpango huo mpana wa kisiasa.Ban Ki Moon pia alieleza kwamba amekuwa akiendesha majadiliano ya kinana wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama, nchi zinazotoa idadi kubwa yawalinda usalama (TCC) na Jumuiya ya Ulaya ( EU).
Akafafanua kwa kusema, majadiliano yake na pande hizo tatu yanalengakatika kutafuta namna ya kuboresha mamlaka ya utekelezaji wa majukumu ya Misheni ya Umoja wa Mataifa ya Kutuliza Amani katika Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO).
" Hali ya kiusalama katika Jamhuri ya Kidemokarasi ya Kongo bado ni tetena hasa katika eneo la Mashariki. Na kwa sababu hiyo, pamoja nakuwasiliana n amarais niliowataja, nimekuwa nikifanya majadiliano ya kinana Baraza la Usalama, TCC, na EU ili kuangalia namna gani tunaweza kuwana mbinu na mwelekeo tofauti wa kuboresha mamlaka ya MONUSCO ili iwezekuwajibika zaidi" akasema Katibu Mkuu
Na kuongeza nitaendelea na majadiliano haya ili tuweze hatimayekuboresha utendaji wa MONUSCO haraka iwezekanavyo.
Akasema, kwa ujumla MONUSCO imekuwa ikifanya kazi nzuri ya kusimamiaamani na kulinda raia pamoja na maeneo muhimu.
Hata hivyo akasemakuwa wakati mwingine MONUSCO imeshindwa kutekeleza majukumu yakekikamilifu na hasa pale wanaposhindwa kufanya kazi kwa karibu na Jeshi laKitaifa la DRC.
Katika siku za hivi karibuni Misheni hiyo ya MONUSCO na Umoja wa Mataifakwa ujumla imejikuta katika wakati mgumu ikitupiwa lawama kutoka kilakona, kwa kile kinachooneka kwamba imeshindwa kabisa kuleta utulivu wakudumu katika eneo la mashariki ya DRC.
Lawama zaidi zimejitokeza pale kundi la waasi la M23 lilipoweza kuutwa mjiwa GOMA bila ya pingamizi lolote kutoka MONUSCO.
Hali iliyotafsiriwa nawachambuzi wa mambo kwamba, walinda amani hao kuonekana kama vileni watalii zaidi na si askari madhubuti.
Aidha Katibu Mkuu wa UM ameitaka pia Jumuiya ya Kimataifa katika ujumlawake kuwa na mtazamo mpya ya namna ya kushughulikia hali tete yaMashariki ya DRC.
Akasema eneo hilo na eneo la Maziwa Makuu limekumbwa na mgogorompya na hasa baada ya kuibuka kwa kundi la M23.
Kundi ambalo pamojana makundi mengine ya waasi limekuwa likilalamikiwa kwa ukiukwajimkubwa wa haki za binadamu, vikiwamo pia vitendo vya ubakaji kwawanawake.Akasema Ban Ki Moon
" wakati umefika kwa Jumuia ya Kimataifa kuangaliaupya utaratibu wake wa kushughulikia mgogoro wa DRC na Kanda yaMaziwa Makuu. Kwa kuangalia upya sababu za msingi za migogoro nakuzishughulikia kwa kina.
|
TANZANIA KUANDAA WORLD TRAVEL AWARDS 2025 KWA BARA LA AFRIKA – DKT ABBASI
-
Na John Mapepele
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesema Tanzania
inakwenda kuandaa Tuzo za Utalii duniani (World Travel Awards, W...
20 minutes ago
No comments:
Post a Comment