Padre anayejulikana kwa jina la Ambrose Mkenda, inadaiwa amepigwa Risasi na Watu wasiofahamika kwenye wakati akiwa katika geti la nyumbani kwake wakati akiingia nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar, ambako ni makazi, alipokuwa ndani ya gari alilokuwa akiendesha akiwa peke yake.
Kwa mujibu wa taarifa ya Redio One Stereo, iliyotolewa jana, imeelezwa kuwa hali ya Padre huyo kwa sasa bado si nzuri kutokana na risasi hiyo kumjeruhi maeneo ya mdomoni.
Aidha imeelezwa kuwa watu waliofanya tukio hilo walionekana wakiwa katika usafiri wa pikipiki, ambapo walimvamia wakati akisubiri kufunguliwa geti ili kuingia nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment