Habari za Punde

*BALOZI IDDI ATEMBELEA KITUO CHA KUSAMBAZA UMEME NA KUWAFARIJI WALIOUNGULIWA NA NYUMBA ZANZIBAR

 Wahandisi wa Shirika la Umeme Zanzibar { zeco } wakiwa katika jitihada za kurejesha huduma za umeme baada ya kituo cha kusambazia umeme ndani ya mji mkongwe kilichopo Darajani Mjini Zanzibar kupata hitilafu.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar, Hassan Ali, akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif ,wakati alipofanya ziara fupi kuangalia harakati za wahandisi wa shirika la umeme kuondosha hitilafu iliyokikumba kituo cha kusambazia umeme mji mkongwe kilichopo Darajani.
Waweza hisi kuwa huenda mahala hapa amezunguukwa mgonjwa aliye mahututi, akipatiwa huduma ya kwanza, lakini la hasha hapa ni jopo zima la wahandisi wa shirika la umeme Zanzibar, wakiwa bize kuhakikisha huduma za umeme ndani ya eneo la mji mkongwe unarejea mara moja kufuatia kituo cha kusambazia umeme kilichopo Darajani Mjini Zanzibar kupata hitilafu, jana.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili, Juma Ali, akipatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, aliyefika nyumbani kwake Bububu Kijichi kumfajiri baada ya nyumba yake kuungua moto mapema jana asubuhi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.