Mshambuliaji machachari wa Simba, Mrisho Ngasa, akikosa penati katika kipindi cha pili, penati iliyosababishwa na Ramadhan Chombo 'Ledondo' baada ya kuchezewa vibaya na beki wa African Lyon.
Baada ya Mwamuzi wa mchezo huo, Israel Mujuni, kupuliza kipyenga cha kuashiria kuwa ni kwaju wa penati, Mrisho Ngasa, alisogea eneo hilo na kuchukua mpia na kisha kuuweka katika alama ya kupigia penati huku akirudi nyuma.
Baada ya Ngasa, kuuweka mpira huo, Kipa wa African Lyon, Abdul Seif, alisogea na kuuchukua mpira huo na kisha kwenda nao hadi golini na kuurusha jambo ambalo lilimfanya Ngasa, kuanza upya kuutenga mpira huo na kuanza kurudi nyuma kujiandaa kupiga penati hiyo.
Wakati Ngasa, akirudi nyuma, Mashabiki wa Yanga walioketi katika jukwaa la Yanga, walianza kumshangilia Ngasa, hata kabla ya kupiga kwaju huo, kwa makelele na makofi ya pamoja kutoka kwa mashabiki hao, jambo ambalo liliwashangasa mashabiki wa simba, ambao wao waliamua kukaa kimpya hadi ilipopigwa penati hiyo na kupanguliwa na kipa Abdul, na ndiyo ikasikika sauti ya kulaumu kukosa penati hiyo kutoka kwa mashabiki wa Simba, huku mashabiki wa Yanga wakiendelea tu kumshangilia pamoja na kutoka. Haikuweza kufahamika sababu iliyowafanya mashabiki hao kumshangia Ngasa.
Beki wa African Lyon, akiondosha mpira huo uliopanguliwa na kipa wake baada ya Ngasa kukosa penati hiyo.
No comments:
Post a Comment