Habari za Punde

*TAHADHARI YA MVUA KUBWA NCHINI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WIZARA YA UCHUKUZI MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Simu pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 29 Januari, 2013

Taarifa kwa umma: Uwezekano wa matukio ya mvua kubwa
Taarifa Na. 20130129-02
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 12:00 Jioni
Daraja la Taarifa:
1:Taarifa 2:Ushauri
3:Tahadhari
4:Tahadhari Kubwa:
Ushauri
Kuanzia:
Tarehe 30 Januari, 2013
Mpaka:
Tarehe 01 Februari, 2013

Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku)

Kiwango cha uhakika: Wastani
Maeneo yatakayoathirika ni:- 
Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe,
Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani, Mtwara na maeneo jirani na
mikoa hiyo.

Maelezo:
Kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa
Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu
kutoka Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.

Angalizo:
Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavu
wanashauriwa kuchukua tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika
na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.

Maelezo ya Ziada Mamlaka inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na kutoa mrejeo (updates) kila itakapobidi.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.