Habari za Punde

*WANAFUNZI UDOM WAPANGA KUFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO MKOANI MOROGORO MWEZI MACHI

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wamepanga kufanya ziara ya kihistoria mkoani Morogoro mwezi wa tatu mwaka huu.

 Ziara hiyo itakuwa ni ya siku tatu iliyopewa jina la Dom mpaka Moro (Bata kwenda bata kurudi) inatarajia kufanyika sehemu mbalilmbali za mkoa wa Morogoro. 

Akizungumza kwa Njia ya Simu Mratibu wa ziara hiyo, Mr AMANI KIZUGUTO, ameuambia Mtandao huu  kwamba taratibu za awali za maandalizi kwa upande mmoja zimekamilika kwani tayari wameshazungumza na mshauri wa wanafunzi (dean of students) katika maandalizi ya awali. 

Aidha alisema kuwa wanatarajia katika ziara hiyo kutembelea mbuga ya wanyama mikumi, maporomoko ya maji katika milima ya udizungwa, ambapo pia bado wanafanya mazungumzo na wakuu wa Vyuo Vikuu vilivypo mkoani humo, ili katika ziara hiyo waweze kufanya ziara katika vyuo hivyo, ikiwa ni pamoja na kujadiliano masuala ya elimu.

Haya sasa kazi kwenu wana udom kwa wale mtakaopenda kwenda wasilianeni na mratibu kwa simu namba 0717 376735 /0769 081122

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.