1. Kamati ya Uchafguzi ya TFF imepitia mchakato mzima wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Uchaguzi wa Tanzania Premier League Board (TPL Board) ili kujiridhisha kuwa mchakato mzima wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzì na Katiba ya TTF.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa kuna matatizo ya kikanuni ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwanza kabla ya kuendelea na mchakato wa uchaguzi.
2. Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kwa mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Ibara ya 10(5) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF INASITISHA zoezi la uchaguzi wa Tanzania Premier League Board (TPL Board) na Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hadi hapo matatizo hayo ya kikanuni yatakapopata utatuzi.
3. Kamati ya Uchaguzi itawatangazia baadaye tarehe mpya za uchaguzi wa
Tanzania Premier League Board (TPL Board) na Shirikisho la Mpira we Miguu Tanzania (TFF).
Deogratias Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI TFF
No comments:
Post a Comment