Maafisa
tume wafunzwa stadi za uchunguzi
Na
Mbaraka Kambona, Arusha
Mafunzo
hayo ya wiki mbili kuanzia februari 18 hadi februari 28 yanafanyika katika
hoteli ya Palace Arusha iliyopo jijini Arusha na yanaendeshwa kwa ufadhili wa Ubalozi
wa Uholanzi kwa kushirikiana na Center for International for Legal Cooperation
(CILC).
Wakufunzi
katika mafunzo hayo ni Paul Brookes,Mkurugenzi wa Utafiti na Nyaraka wa
tume,Bi.Epiphania Mfundo, Profesa Martin Kuijer na Steven Mubiru.
Akifungua
mkutano huo,Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Mhe.Jaji
Kiongozi(mstaafu)Amiri Manento alisema kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni
kuwaongezea stadi za uchunguzi maafisa hao ili waweze kufanya uchunguzi wao kwa
ufanisi na kwa wakati pamoja na kupata wakufunzi.
‘’Hivyo
ni ni matumaini yangu mafunzo haya yatawapa vitendea kazi bora
vitakavyowawezesha kutimiza malengo ya tume kwa wakati’’,aliongeza
Aidha,aliwakumbusha
washiriki kuwa Tume imepewa mamlaka makubwa ya kikatiba na kisheria ya
kuhamasisha,kulinda na kuhifadhi haki za binadamu na misingi ya utawala bora
nchini.
‘’kwa mamlaka haya,ni wazi kuwa Tume ina jukumu
kubwa la kulinda watu dhidi ya uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi
ya utawala bora’’,alisistiza
Ubalozi
wa Uholanzi nchini pamoja na Tume walikubaliana kufanya mafunzo haya kwa pamoja
ili kukuza ujuzi na stadi za kiuchunguzi wa kwa maafisa wa Tume ili kuwaongezea
uwezo wakati wa kutekeleza majukumu yao.
No comments:
Post a Comment