Habari za Punde

*MAONI YA WADAU KUHUSU WEZI WA KAZI ZA WATU 'MABLOGGER'

Ahmad Michuzi:- ASANTEEEE...! MIMI NILIISHASEMA SANA KUHUSU HILI JAMBO,NAONA TUSHIRIKIANE TU KUHIMIZANA KUWA WABUNIFU NA KUJITUMA,TUACHE TABIA YA MLO MMOJA BILA YA KUONGEZA MATUNDA,MATOKEO YAKE TUTAKOSA AFYA NA KUANZA KUCHEKWA HUKO NJE,MLO MMOJA TUONGEZE NA MATUNDA ILI KUJENGA AFYA,SUALA LA TUNDA LIPI WEWE NDIYE UTAKAEAMUA,LIPI LINAKUFAA.

Joseph Lukaza:- asante sana na wewe kwa kutoa lililola moyoni sufiani maana sisi wengine tushaliongelea sana hadi kufikia hatua ya kuchukiwa na baadhi ya watu wenye blogs hizo za kukopy na kupaste.Inaweza kuisaidia pia.Mfano jana Nimepiga picha kuhusu wafuasi wa Shekhe Ponda kisutu Sekunde tu nishaziona Sehemu tena Bila hata Credit 

Issa Michuzi:- Pamoja na kwamba sitaki kuchukua upande katika hili, ila naungana mkono na Mbeya Yetu.

Na kwa kuwa wote letu ni kupasha habari iko haja kuketi na kutafakari maana tusigombee  fito wakati tunajenga nyumba moja. 

Ni kweli inakatisha tamaa ila mie binafasi niliacha kulalama siku kibao kwani nilikuja kumaizi kwamba anayenyofoa kazi yangu hunipromoti pia. 

Yaani msomaji akiikuta habari aliyoiona kwangu harudi tena kwa aliyeCopy kwanini asipate vitu original?

Pia kaka Sufiani wewe (na mimi na wengine tunaofanya kazi ofisi za umma) ulitakiwa uwe wa mwisho kulalama, maana kama alivyosema Mbeya Yetu, kama ukiacha kutuma picha za Mkuu itasaidia nini?

Cha msingi hapa ni kulazimisha kila anyetumia kazi ya mtu aseme alikoitoa. kinyume cha hapo huyo ni mwizi na mgomvi nasi tutamtenga. 

hayo ni mawazo yangu binfasi ila nangoja toka kwa wengine.
MM

Mbeya Yetu:- Asante kwa ujumbe wako lakini kumbuka ulimwengu wa dijitali ni tofauti na ulimwengu wa analojia wa magazeti

Mbeya yetu haiungani na ujumbe ulio andika kwa jazba. Na tunapenda kusema tuu kama ushauri kwamba kama unaona kazi zako zinaibiwa basi weka water mark katikati ya picha kisha pale chini andika ukitaka picha isiyo na watermark wawasiliane nawe.

Pia jambo jengine la msingi ni kwamba habari hizi umelalamika za kufanana basi tunaomba na wewe ili kuondoa hilo usiwe unatuma story mfano zinazofanana kwa  bloggers wengine hii itasaidia sana, hawa wa kukopy na kupaste kila siku ndo story hii hii tuu. 

Ukitaka ku fight fanya mambo kwa akili na si kwa kutumia maguvu . Weka water mark tuu mwisho kabisa sisi sote lengo ni moja kufikisha ujumbe

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.