Habari za Punde

*MWANAFUNZI WA MAKONGO ASHINDA VITZ YA VALENTINE


Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo baada ya kupatikana kwa washindi wa ‘Valentine Campaign’ ambapo Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Makongo, Mudhir Ndonya alishinda gari aina ya Vitz lenye thamani y ash milioni 8. Picha na Mpiga picha wetu.
*****************************
Na Mwandishi wetu
MWANAFUNZI wa  shule ya Sekondari ya Makongo, Mudhir Ndonya (20) ameshinda zawadi ya gari aina ya Vitz kufuatia shindano la siku ya wapendanao (Valentine campaign) lililomalizika Februari 14.
Mbali ya droo ya Vitz lenye thamani ya sh Milioni 8, pia washindi mbali mbali walipatikana katika siku ya mwisho wa shindano hilo lililofanyika kwenye ofisi za African Media Group (AMG).
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Push Media Mobile Rodney Rugambo alisema kuwa Ndonya ameibuka mshindi  baada ya namba yake kuibuka ya kwanza katika shindano hilo lililodumu kwa takribani miazi mitatu na kutumia zaidi ya sh milioni 30.
Rugambo alisema kuwa wahsindi wengine katika droo hiyo ni Daudi Samson (22) ambaye pia ni mwanafunzi aliyejishindia Ipad, Tabia Lihonde (44) ambaye ni nesi anayefanya kazi Mtwara na kuibuka mshindi wa simu ya mkononi aina ya blackberry na Emmanuel Sanga aliyeshinda home theare.
Akizungumza kwa baada ya ushindi huo, Ndonya alisema kuwa amefurahi sana kwani ndoto yake ya kushinda gari imetimia.
“Nilishiriki katika shindano kama washindani wengine, ndoto yangu ilikuwa ni kushinda, nashukuru nimeshinda na ushindi huu ni chachu ya kuendelea kushiriki katika mashindano mengine yajayo, ” alisema  Ndonya. 
Mbali ya Push Media Mobile, droo hiyo pia iliendeshwa na kituo cha televisheni cha Channel Ten na Radio ya Magic FM na kudhaminiwa na Alliance Insurance.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.