Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akimtoka mchezaji wa Azam Fc, Hamis Mcha, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Niyonzima katika dakika ya 32 akiunganisha pasi nzuri kutoka kwa Jerry Tegete, ambaye kwa leo ameonekana kupwaya zaidi na kukosa mabao kama matatu ya wazi.
Kwa ushindi huo Sasa Yanga inaongoza Ligi hiyo kwa kuwa na jumla ya Pointi 39, wakifuatiwa na Azam wenye Pointi 36, nafasi ya tatu inashikiliwa na Simba wakiwa na Pointi 31 nafasi ya nne ni Coast Union wenye Pointi 30, huku Yanga wakiwa na mchezo mmoja kibindoni.
Baada ya mchezo huo kumalizika wachezaji wa Azam, walimzonga mwamuzi wa mchezo huo kwa kile walichodai kuonewa sakata lililookolewa na askari wa usalam kwa kuwaondoa waamuzi hao uwanjani wakiwa chini ya ulinzi mkali huku wakipondwa na chupa za mikojo.
Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, akijilaumu baada ya kukosa bao la wazi.
Mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete (kuli) akijaribu kumchambua kipa wa Azam Fc, Mwadin Ally, wakati wa mchezo huo, ambapo Tegete alikosa baada ya kipa huyo kuudaka mpira huo.
WATANI WA JADI BWANA!!!!, Mashabiki wa Yanga, wakiwakebehi watani wao Mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia Azam Fc, kwa Bango lenye Ujumbe huu. ''Msomaji soma mwenyewe''.
Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichoanza.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga, waliojitokeza kuishangilia timu yao leo, ambao wanakadiliwa kuwa kama 25,0000 hivi.
Kikosi cha Azam Fc, kilichoanza. Katika michezo mingine ya Ligi Kuu Tanzania Prisons na Polisi Moro, zimetoka suluhu 0-0, Mgambo 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.
No comments:
Post a Comment