Habari za Punde

*BONDIA AMOUR MZUNGU ATAMBA KUMCHAPA MARWA


Bondia mwenye makazi yake kisiwani unguja. Amour said, 'Mzungu' (kushoto)  ametamba kumsambaratisha bondia mwenzake Mkongwe Joseph Marwa, na kumstaafisha mchezo huo.
Mzungu, amesema kuwa atahakikisha anastaafisha mchezo huo Bondia Marwa  aliyewahi kuwa tishio na kuchukua medali nyingi tofauti tofauti katika ngumi za ridhaa na kuwa bingwa katika ngumi za kulipwa.
Mabondia hao watakutana Ulingoni katika  pambano litakalofanyika katika ukumbi wa  CCM Mwinjuma-Mwananyamala, April  7 mwaka huu.
Mzungu aliendelea kumnanga Marwa kuwa kwa sasa hivi bondia huyo tayari  umri umekwenda na anakili kuwa Marwa, ndiye aliyemkaribisha katika ngumi na sasa ameamua kumstaafisha mwalimu wake huyo.
Mzungu amesema kuwa hivi sasa yeye ndiye atakuwa mwalimu wa mwalimu wake kwa kumfundisha kwa kumchapa bila huruma, ambapo alisema kuwa baada ya kumstaafisha Marwa, amepanga kumtafuta Mchumiatumbo ili kuonyesha kuwa bora katika ngumi za uzito wa juu.
Pambano la Amour Mzungu na Joseph Marwa litakuwa ni la raundi nane kuwasindikiza wadogo zao wanaochipukia  kwa kasi Issa Omar na Shaban Madilu watakaocheza raundi kumi za ubingwa wa taifa wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO),Ambao upo wazi kugombaniwa na mabondia hao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.