Habari za Punde

*MABONDIA WA DAR KUONYESHANA KAZI NA MABONDIA WA MUHEZA KATIKA VIWANJA VYA JITEGEMEE MUHEZA TANGA

BONDIA Iddy Mkwela wa Dar es salaam, anatarajia kuoneshana kazi ya na Lucas Ndula wa Muheza wakati wa kusherekea sikukuu za pasaka jumapili ya march 31 katika viwanja vya wazi vya Jitegemee vilivyopo wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa mpambano huo wa raundi 6 kg,60 bondia wa siku nyingi ambae kwa sasa ni kocha wa mchezo huo Muheza, Chalres Muhilu ' Spins' alisema mpambano huo wa wazi umeandaliwa kwa ajili ya kutoa burudani wilayani hapo na kuhamasisha mchezo wa masumbwi

Katika mchezo huo kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi yatakayoanza saa kumi jioni ambapo hakutakuwa na viingilio.

Wapenzi wa mchezo huo wametakiwa kujitokeza kushuhudia mabondia kutoka Dar wakipambana na Muheza pamoja na kutoa rai kujitokeza kwa wafadhili kudhamini mchezo huo unaopendwa na vijana wengi wilayani humo.

Naye Kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' aliyepewa jukumu la kwenda na vijana kutoka Dar kutoa hamasa ya mchezo huo, amesema ataongozana mabondia, Nassoro Mbwiga, atakayemenyana na Bakari Sendekwa katika uzito wa kilo 52 na Iddy Mkwela atakaepambana na Lucas Ndula mpambano wa raundi 6.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.